Sehemu ya watumishi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wakiwa ndani ya Mapango ya Amboni
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngongoro wakicheza bao wakati wa ziara yao ya kutembelea Mapango ya Amboni
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wakiwa eneo la Mapango ya Amboni
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wakiwa eneo la Mapango ya Amboni
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wakitoka ndani ya Mapango ya Amboni
MAMLAKA ya Hifadhi ya Ngorogoro imesema kwamba kumefanyika maboresho makubwa na Serikali kwenye Mapango ya Amboni yaliyopo Jijini Tanga ikiwemo kufungwa taa zaidi ya 30 ambazo ukiingia kila hatua unakutana nazo ambazo zinakuwezesha kuona mbele ili kuwawezesha watalii wa ndani na nje kuweza kuona vizuri uzuri na upekee wa Mapango hayo.
Hayo yalisemwa na Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Kassim Nyaki wakati wachezaji wa Mamlaka hiyo wanaoshiriki mashindano ya Shimuta walipokwenda kutembelea mapango hayo ambapo alisema wamefanya hivyo kama sehemu ya kufahamasisha utalii wa mapango hayo ya Amboni Tanga.
Ambapo alisema uwepo wa taa hizo unawezesha watalii wa ndani na nje kuweza kuona mbele watalii wanaofika wanaweza kuona uzuri na upekee wa mapango hayo yaliyosheheni historia mbalimbali zenye kuvutia.
Alisema zamani ulikuwa ukiingia kwenye mapango hayo kipindi cha mvua chini kuna loa kama matope lakini kwa sasa wamepanga matofali kumuwezesha mtalii asipate shida ya kutembelea mapango hayo kipindi cha mvua hivyo kwao ni fursa.
“Vivutio vinavyopatikana madhari tulivu ya mapanga,sehemu ambayo inasemekana mzungu mmoja na mkewe na mbwa walitumbukia na hawajaweza kutokea tena lakini kuna sehemu kuna michoro ya vitabu vya dini kama vile biblia na kiirabu hayo maneneo hayakuandikiwa na mtu ni asili”Alisema Afisa Uhusiano huyo.
Alisema pia kuna sehemu ina ishara ya msikiti na alama ambazo unaziona za kanisani kama bikira maria eneo lenye muundo wa meli au boti ikiwemo jiwe ambalo limejichonga wenyewe kama tembo huku akieleza wanahamasisha watanzania wote waende kuona upekee na hawatajuta kufika kwenye mapango hayo.
‘Lakini pia michezo inakwenda sambamba na utalii hivyo ni sehemu ya kuhamaisha utalii wa ndani utaona mapango ya Amboni tokea yalivyokasimishwa kwetu hivyo kuna maboresha makubwa yamefanyika ikiwemo barabara kupitika vizuri”Alisema
Aidha alisema pia huko nyuma mtu ulikuwa ukiingia kwenye mapango hayo alikuwa ukikutana na giza totoro lakini kwa sasa maboresho yaliyofanywa na serikali ni kuwekwa taa kuna taa zaidi ya 30 zipo ndani ukiingia kila hatua fulani kuna taa ambayo inakuwezesha
“Watanzania watenge muda siku moja waje Tanga kuja kutembelea mapango ya Amboni na ni kilomita 9 kutoka Katikati ya Jiji kufika eneo hilo na kuweza kuona upekee wa mapango hayo”Alisema
Hata hivyo Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro alisema tokea walipokabidhiwa na serikali kuyasimamia mapango hayo kumekuwa na maboresho mengi ambayo yamekuwa na tija.
Afisa Uhusiano hayo alisema timu za Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorogoro zimekuja kushiriki kwenye michezo ya shimuta 2020 pamoja na kuja kwenye michezo lakini wao kazi yao kubwa ni utalii.
Alieleza hivyo wao kama wanavyojua mapango ya amboni Tanga ni eneo ambalo lilikasimiwa kwa mamlaka hiyo kwa ajili ya kuliendeleza na kulitunza.
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkuu wa Kanda ya Mapango ya Amboni Tanga Mecksadeck Maximilian aliwataka wenyeji wa mkoa wa Tanga hutumia maeneo hayo kama tambuko na mzimu mkubwa unaotambulika na mzimu wa mababu wanayatumia kama sehemu ya kuabudu na kuomba dua na kufanikiwa.
Alieleza mapango hayo hivi sasa yapo chini ya Hifadhi ya Mamlaka ya Ngorongoro na tokea walipokabidhiwa cha kwanza walichofanya kuhakikisha usalama na ulinzi kwenye mapango hayo kutokana na utalii ni starehe .
Alisema lakini silaha ya kwanza katika utalii duniani ni usalama mtu anapokuja watahakikisha anakuwa salama na wapo wamehakikisha eneo lipo salama kila wakati.
“Huko ndani ya Mapango ni eneo kubwa sana inawezekana kunaweza kutokea nyoka hivyo tukaona tufunge taa ambazo mtu akiingia taa zinawaka na kukiwa hakuna mtu kuna kuwa ni kiza ili kutokuathiri uhalisia wa mapango hayo”Alisema
Hata hivyo alisema kinachoendelea hivi sasa ni uwepo wa wahandisi wa Tarura ambao wameshaawaalika wanajenga eneo la kupumzukia wageni na kupata chakula na eneo ambalo litatumika kuweke magari na baada ya wiki mbili au tatu wataweka mabango.