Home Mchanganyiko MWENYEKITI WA BODI YA TAWA ATEMBELEA MAPORI YA AKIBA YA IKORONGO NA...

MWENYEKITI WA BODI YA TAWA ATEMBELEA MAPORI YA AKIBA YA IKORONGO NA GRUMETI WILAYANI SERENGETI

0

  

………………………………………………………………………………………..

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Mej.Gen(Mstaafu) Hamisi Senfuko akiongozana na wajumbe wa Bodi,Menejimenti ya Tawa Makao Makuu ikiongozwa na Kaimu Kamishna wa TAWA Bw.Mabula Misungwi Nyanda pamoja na uongozi wa mapori hayo jana tarehe 26/11/2020 wamefanya ziara ya kutembelea vivutio vya utalii katika Mapori hayo

Aidha, Mej.Gen(Mstaafu) Semfuko amefanya kikao na watumishi wa mapori hayo Kwa kuwataka kuzingatia masuala mbalimbali ya Uhifadhi yskiwemo;
# Kufanya kazi kwa bidii na kujituma ili kuongeza mapato hasa kutokana na shughuli za uwindaji wa kitalii Kwa kuzingatia hotuba ya Mhe.Rais John Pombe Magufuli wakati wa uzinduzi wa Bunge la 12 laJanhuri ya Muungano wa Tanzania
#Watumishi wawe wepesi sana katika kutumia lugha ya Biashara kuhakikisha wanavutia wawekezaji katika kuongeza mapato ya utalii
#Mapori ya Akiba ya Ikorongo /Grumeti na Maswa yawe ni mapori ya mfano kwa kuvutia wawekezaji katika TAWA ná Tanzania Kwa jumla Kwa kuwataka watumishi wafanye kazi Kwa uadilifu.

Aidha,katika kikao hicho kulifanyika wasilisho la maeneo maalumu ya uwekezaji
ambayo yako 13, lakini ambayo yameshachukuliwa na wawekezaji yako 6 yakiwepo mapori ya Akiba ya Ikorongo na Grumeti.Wasilisho hilo lilifanywa na Naibu Kamishna wa Huduma za Utalii na Biashara Bw.Imani Nkuwi.

Sambamba na ziara hiyo Menejimenti ya mapori hayo waliwasilisha changamoto zao ikiwa ni pamoja na ;

Kutokuwepo umeme wa uhakika, uhaba wa magari , uhaba wa nyumba za watumishi pamoja na shida ya upatikanaji wa maji safi.

Mwenyekiti ameahidi atashitikiana na Menejimenti ya TAWA kutatua changamoto hizo.