MABINGWA watetezi, Bayern Munich wamejihakikishia kwenda Hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa baada ya ushindi wa 3-1 dhidi ya RB Salzburg katika mchezo wa Kundi A usiku wa jana Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich. Mabao ya Bayern Munich yalifungwa na Robert Lewandowski dakika ya 42, Maximilian Wober aliyejifunga dakika ya 52 na Leroy Sane dakika ya 68, wakati la RB Salzburg lilifungwa na Mergim Berisha dakika ya 73. Bayern Munich inafikisha pointi 12 na kuendelea kuongoza kundi hilo kwa pointi saba zaidi ya Atletico Madrid, wakati RB Salzburg inaendelea kushika mkia kwa pointi yake mmoja, nyuma ya Lokomotiv Moscow yenye pointi tatu kuelekea mechi za mwisho PICHA ZAIDI SOMA HAPA
BAYERN MUNICH YATINGA 16 BORA YAICHAPA 3-1 RB SALZBURG LIGI YA MABINGWA
By Alex Sonna
November 26, 2020 | 6:05 am

Related Stories
View all
Michezo
1 hour ago
MALIASILI YAISULUBU HAKI 41-7, SHIMIWI 2026
Na Sixmund Begashe, Moshi TIMU ya Maliasi Sports Club ya mpira wa Pete KE imeaikandamiza timu ya Haki KE ya Tume ya Haki na…
Michezo
3 days ago
“NMB THE GOAT” ATAMBA MBIO ZA MBUZI, AMSHINDA MPINZANI WA BOWMAN
Mbuzi wa Benki ya NMB, ‘NMB the GOAT’, ameibuka mshindi katika mbio za ‘NMB unGOATable Race’ zilizofanyika Septemba 19, 2026, akimshinda mbuzi wa Bowman…
