Home Michezo TIMU ZA NCAA ZATINGA NUSU FAINALI MASHINDANO WA SHIMMUTA TANGA

TIMU ZA NCAA ZATINGA NUSU FAINALI MASHINDANO WA SHIMMUTA TANGA

0

Kikosi cha timu ya Mpira wa Miguu cha timu ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kilichoitoa timu ya mpira wa miguu ya Chuo Kikuu cha Dodoma na kufanikiwa kutinga hatua ya Nusu fainali katika mashindano ya SHIMMUTA yanayoendelea jijini Tanga.

Timu ya wanawake inayoshiriki mchezo wa kamba ya NCAA ikiwa katika picha ya pamoja baada ya kuifunga timu ya kamba ya Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) katika mashindano ya SHIMMUTA yanayoendelea jijini Tanga na kufanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali.

Kikosi cha timu ya mpira wa pete ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro inayoshiriki mashindano ya SHIMMUTA jijini Tanga.

 …………………………………………………………………………………………..

Na Kassim Nyaki-NCAA Tanga.

Timu za Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) zinazoshiriki mashindano ya  Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma  Taasisi na Makampuni binafsi Tanzania (SHIMMUTA) zimeendelea kufanya vizuri katika mashindano hayo na kufuzu hatua nusu fainali.

Timu ya mpira wa miguu ya NCAA ambayo imeshinda mechi zake mfulullizo tangu mashindano hayo yaanze, jana iliifunga timu ya Reli Tanga kwa magoli 3-0 na kuiwezesha kuingia hatua ya robo fainali. Aidha katika mchezo wa robo fainali uliochezwa leo tarehe 25 /11/2020 NCAA ilifunga timu ya Chuo kikuu cha Dodoma goli 1-0 na kufanikiwa kufuzu katika hatua ya nusu fainali ambapo itakutana na timu ya Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA).

Kwa upande wa mchezo wa Kuvuta kamba timu ya wanawake ya NCAA imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuitoa timu ya wanawake kutoka Chuo cha Teknolojia Dar es Salaam (DIT) kwa ushindi wa seti 2-0.

Timu ya mpira wa wavu (Volleyball)  na timu ya mpira wa pete za NCAA ambazo zilifuzu hatua ya kucheza nusu fainali zimepoteza mechi zake leo dhidi ya NHIF na TANESCO ambapo baada ya matokeo hayo timu hizo zinasubiri kucheza mechi za kutafuta mshindi wa tatu katika mashindano hayo.

Mashindano hayo ambayo yalianza tarehe 16 Novemba, 2020  yanatarajiwa kuhitimishwa tarehe 29 Novemba, 2020 Jijini Tanga.