MBUNGE wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa kikao cha Uchaguzi wa mgombea nafasi ya
Meya wa Jiji la Tanga

Meya Mpya Mstahiki Abdurahman Shillow akizungumza katika kikao hicho mara baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo

Meza
kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye uchaguzi huo katikati ni
Mbunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia ni Mbunge wa Viti
Maalumu Mkoa wa Tanga Mhandisi Mwanaisha Ulenge  na kushoto ni Mkuu wa
wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Mkoba akizungumza na waheshimiwa madiwani kabla ya kuanza uchaguzi huo

Mbunge
wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia akiwa na Mstahiki Meya mpya
wa Jijini la Tanga (CCM) Abdurahaman Shillow kushoto na anayefuatia ni
Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Tanga (CCM) Mhandisi
Mwanaisha Ulenge

Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini, Mhe Ummy Mwalimu amehimiza umoja na mshikamano baina ya madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Tanga ili kuweza kuwatumikia vyema wananchi wa Jiji la Tanga.
Mhe Ummy ameyasema hayo leo katika kikao cha Uchaguzi wa mgombea nafasi ya Meya wa Jiji la Tanga ambapo ameeleza  kuwa uchaguzi umekwisha na wananchi wa Tanga Mjini wamewaamini  kwa kuwapa ushindi mkubwa kwa mgombea Urais, Ubunge na Madiwani wa CCM katika kata zote 27 za Tanga Mjini.
Alisema baada ya uchaguzi huo kumalizika viongozi hao wana wajibu wa kuwatumikia wananchi wa Tanga mjini bila kuchoka ili kuleta maendeleo yao na hatimaye kuweza kuchochea kasi ya ukuaji wa uchumi.
Mhe Ummy amempongeza Meya Mpya Mstahiki Abdurahman Shillow kwa kuaminiwa kuwa Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga huku akihaidi kumpa ushirikiano wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake.
Katika uchaguzi huo uliofanyika leo katika Ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa Tanga ulisimamiwa na Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa.
Akitangaza matokeo hayo Mwilapwa alimtangaza Mhe Abdurahmani Shillow ambaye ni Diwani wa  Kata ya Mzingani ambaye ni  mgombea Umeya wa Jiji la Tanga kwa kupata kura 26 huku nafasi ya pili ikienda kwa  Mhe Said Mbaruku ambae amepata kura 11 wakati Mhe Ahmed Mwinjanga amepata kura 1 katika idadi ya  wapigakura walikuwa 38.