Spika wa bunge Job Ndugai akipokea karatasi yenye jina la kupendekezwa kwa Waziri Mkuu wa Tanzania kutoka kwa Mpambe wa Rais .

Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania  Job Ndugai akionyesha karatasi yenye jina la kupendekezwa kwa  Waziri Mkuu baada ya kupokea kutoka kwa mpambe wa Rais 

Spika wa bunge Job Ndugai akisaini karatasi yenye jina la kumpendekeza Waziri Mkuu wa Tanzania baada ya kukabidhiwa na Mpambe wa Rais 

Baadhi ya wabunge wa wakimpongeza Kassim Majaliwa baada ya jina lake kupendekezwa na Rais Dkt.Magufuli kushika nafasi ya Uwaziri Mkuu

…………………………………………………………………………..

Na.Alex Sonna,Dodoma

Mbunge wa Ruangwa, Kassim Majaliwa amependekezwa na Rais Dk John Magufuli kushika nafasi ya Uwaziri Mkuu kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Majaliwa ndie alikua Waziri Mkuu katika awamu ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano na sasa amependekezwa tena.