…………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Dodoma
MBUNGE wa Makete Mhe.Festo Sanga amewaomba watanzania wote kuiombea Dua na Sara Timu ya Taifa ‘Taifa Stars ambayo itashuka uwanjani kesho kucheza na wenyeji Timu ya Taifa ya Tunisia wa kuwania nafasi ya kufuzu Michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwaka 2021.
Pia amewataka wachezaji wa Taifa Stars kuweka uzalendo mbele ili waweze kupata ushindi kabla yab kurudiana Novemba 17 mwaka huu uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam
Timu ya Taifa Stars kabla ya jana kutua nchini Tunisia waliweka kambi ya muda mfupi nchini Uturuki kujiandaa na mchezo huo utakaofanyika nchini Tunisia kesho Novemba 13 majira ya saa nne usiku kwa saa za Tanzania.
Mhe.Sanga amesema kuwa ana matumaini na kikosi hicho kutokana na kuwa na wachezaji wazoefu kwenye Mashindano mbalimbali ya Kimataifa licha ya kumkosa Nahodha , Mbwana Samatta ambaye ana majeruhi huku akiwataka watanzania kuiombea dua timu yao ili iweze kufanya vizuri.
Aidha Mhe.Sanga amezitaka timu za Simba na Namungo kujiandaa kikamilifu na kuwafatilia wapinzani wao kwenye Michuano ya CAF kwa kuwaanda wachezaji wao katika hali nzuri ya kiushindani zaidi.
” Mimi nimekwua kwenye mpira kwa muda mrefu kwa Timu kama Simba,Namungo, Simba na Timu za Zanzibar Mlandege SC,KVZ FC hii Michuano ya klabu bingwa na Shirikisho Afrika bado tupo nyuma sana hivyo yanatakiwa maandalizi yafanyiki mapema , Simba sina shaka nayo sana ni wazoefu na wamekuwa wakifanya vizuri mara kwa mara lakini pia tunawaomba wajiandae,” Amesema Sanga.
Shirikisho la Afrika CAF limetoa ratiba ya Michuano ya klabu bingwa huku Simba itaanza ugenini na Plateau United ya Nigeria katika Raundi ya Awali huku mabingwa wa Zanzibar, Mlandege SC wataanzia nyumbani dhidi ya mabingwa wa zamani wa michuano hiyo, CS Sfaxien ya Tunisia.
Huku timu ya Namungo FC ya Ruangwa mkoani Lindi itamenyana na Al Rabita FC ya Sudan Kusini, wakati KVZ FC ya Zanzibar itamenyana na El Amal ya Sudan mechi za kwanza zitachezwa kati ya Novemba 27 na 29 na marudiano Desemba 4 hadi 6 mwaka.
Kabla hajaenda kugombea ubunge Mhe.Sanga alikuwa Mkurugunzi wa Singida United na walifanikiwa kuleta wachezaji bora pindi akiwa kiongozi na Kikosi cha Singida kilileta ushindani Mkubwa kwa Ligi Kuu ya Tanzania na wakitinga hatua ya Fainali Michuano ya Kombe la Azam Sport Federedation.