Chama  Tadea kimesema ni vyema mashirika ya haki za binadamu  yakatoa taarifa za  kuwaonya wanasiasa  wanapotoa matamshi  ya kuhatarisha amani na  kutozishutumu serikali zikizo madarakani.
Pia kimesisitiza si haki na si wajibu kwa mashirika hayo kuonekana yakijiegemeza kwenye lawama na kuacha kutoa ushauri mapema.
Makamo Mwenyekiti wa ADA Tadea Juma Ali Khatib ameeleza hayo  kufuatia taarifa iliotolewa na kamisheni ya haki za binadamu zilizodai kuna watu  150 wamekamatwa na polisi.
Khatib  amesema  zipo kauli za baadhi ya viongozi  wa upinzani  ambazo ziliekekeza moja kwa moja kutaka  yatokee machafuko,fujo na uvunjifu  wa amani. 
Amesema pamoja na mashirika ya haki za binadamu  kuwepo yamefumba macho na kutosikika yakilaani au kuonya 
Amesema mtindo wa kujiegemeza katika muktadha wa kulaumu  kuliko kuasa na kuonya mapema hakuonyeshi haki na usawa.
Khatib amesema kutoushutumu upinzani nako  hakuutoshi kukuza ufanusi badala yake yasimame kati kati ili kuonyesha utendaji wenye mizania.
Hata hivyo Katibu mkuu wa Wizara ya Sheria na Katiba ya SMT , Profesa Sifuni Mchome amesema Serikali haijapata taarifa hiyo na huenda hao wamekamatwa kisheria
Taarifa iliyotolewa na shirika la Umoja wa Mataifa na Kamishina wa Shirika la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na Michelle Bachelet limedai viongozi wa upinzani na wafuasi wao wamekamatwa  Oktoba 27.
Michelle amesema  watu haovwametiwa mbaroni siku moja kabla ya kupiga kura na kuelezea wanavyosikitishwa.

Serikali kupitia Profesa Mchome imesema bado haijapata taarifa hiyo na kama ni madai ya watu kukamatwa ni kwa mujibu wa sheria si vinginevyo.