Home Mchanganyiko WATUMISHI TAMISEMI WAPATIWA MAFUNZO YA AFUA ZA VIRUSI VYA UKIMWI

WATUMISHI TAMISEMI WAPATIWA MAFUNZO YA AFUA ZA VIRUSI VYA UKIMWI

0
Muonekano wa Watumishi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) wakiwa ndani ya basi darasa wakifatilia kwa makini mafunzo ya afua za virusi vya UKIMWI mahali pa kazi yanayotolewa na taasisi binafsi ya Tanzania Youth Alliance (TAYOA) kwa njia ya basi darasa leo Jijini Dodoma.
Watumishi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kupatiwa mafunzo ya afua za virusi vya UKIMWI mahali pa kazi yanayotolewa na taasisi binafsi ya Tanzania Youth Alliance (TAYOA) kwa njia ya basi darasa leo Jijini Dodoma.
………………………………………………………
Na. Majid Abdulkarim – Dodoma
Watumishi wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI) wamepatiwa mafunzo ya afua za virusi vya UKIMWI mahali pa kazi yanayotolewa na taasisi binafsi ya Tanzania Youth Alliance (TAYOA) kwa njia ya basi darasa.
Mafunzo hayo yamefanyika leo Jijini Dodoma kwa njia ya basi darasa ambapo mada zilizotolewa katika basi hilo ni Saratani ya Kizazi, Ukweli kuhusu Virusi vya Ukimwi na magonjwa ya ngono, Ukatili wa kijinsi na magonjwa yasioambukizwa.
Aidha mmoja wa Watumishi kutoka Idara ya Serikali za Mitaa, Bw. Brian Samweli amesema kuwa basi darasa limewasaidia kuwa na uelewa zaidi juu ya umuhimu wa kuwa na utamaduni wa kupima Afya zao mara kwa mara ili kupata hali ya afya zao kutokana na wataalam wa afya watakavyo kuwa wamewaelekeza baada ya kupima.
“Tukiwa na utamaduni wa kupima afya zetu katika hospitali na vituo vyetu vya afya itasaidia kujua hali ya afya zetu jambo litakalosaidia kuwahi kupata tiba haraka iwapo utagundulika kuwa na changamoto ya kiafya”, amesema Samweli.
Naye afisa mradi wa timiza malengo Ekinala Kasobile ameeleza kuwa kwa sasa mradi huu unatekelezwa katika mikoa miwili ambayo ni Mkoa wa Dodoma na Morogoro.
“Awali mradi huu ulikuwa unatekelezwa katika halmashauri za Bahi, Kongwa, Kondoa na Mpwapwa kwa lengo la kuifikia jamii ya ndani ya shule na nje ya shule ili kuhakikisha vijana wanatimiza ndoto zao katika maisha yao”, ameeleza Kasobile