Home Siasa KAMATI YA USHINDI YA UWT WILAYA YA DODOMA MJINI YAKUTANA NA MAWAKALA...

KAMATI YA USHINDI YA UWT WILAYA YA DODOMA MJINI YAKUTANA NA MAWAKALA WA MABASI YA NANE NANE

0
Na.Mwandishi Wetu,Dodoma
 Kamati Maalum ya jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) ,Wilaya ya Dodoma Mjini kimeendelea na ziara yake na leo wamekutana na kufanya mazungumzo na Mawakala wa usafirishaji wa Mabasi katika kituo kikuu Cha mabasi  Nane nane kilichopo jijini Dodoma.
Katika  kikao hicho mawakala wamesema kuwa wamefurahishwa na  kazi nzuri ya Mgombea Urais wa CCM Dkt. Magufuli ambaye amejenga stendi hiyo kubwa ya kimataifa ambayo imetoa ajira kwa vijana wengi  wakiwemo mawakala hao wa mabasi.
Aidha kamati hiyo imekutana na  wajasiriamali waliopo katika stendi hiyo na wamemshukuru Rais kwa kuwapatia vitambulisho vya mjasiriamali ambavyo wamelipia pesa kidogo  tofauti na awali walivyokuwa wanatozwa kodi kubwa.
Hata hivyo  Katibu wa UWT Wilaya Diana Madukwa amewaomba  mawakala hao kumchagua Dkt Magufuli kutokana na utendaji kazi wake hivyo ataendeleza kuleta maendeleo kwa wanadodoma pamoja na kwa watanzania.