Home Mchanganyiko WATANO WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA MOTO PUGU STESHENI JIJINI DAR ES...

WATANO WAFARIKI DUNIA KWA AJALI YA MOTO PUGU STESHENI JIJINI DAR ES SALAAM

0

**********************************

NA JAMES SALVATORY

Watu wa tano wa familia moja wakazi wa Kata ya Pugu Stesheni Manispaa ya Ilala Jijini Dar es salaam wamefariki Dunia usiku wa kuamkia leo kwa ajali ya moto.

Imeelezwa ajali hiyo ambayo imetokea katika nyumba ya Edward Jeremia Katemi ambaye ndiye baba wa familia hiyo imesababishwa na hitilafu za umeme majira ya saa nne za usiku.

Akizungumza katika eneo la tukio  jijini Dar es salaam Edward Katemi amesema waliofariki katika ajali hiyo ni pamoja na Mke wake Jackline Frenk,Mdogo wake Ester Katemi,na watoto wake watatu Edwin Katemi,Edsoni Katemi pamoja na Eivon Katemi.

Kamanda msaidia wa Jeshi la Polisi ACP Janet Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema familia hiyo ya watu watano wamefariki kwa ajali hiyo ya moto Zaidi anaeleza.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Pugu stesheni Shukuru Mohamedi Mwinjuma amesema alipokea taarifa majira ya saa saba usiku kutoka kwa mwananchi wake kuwa nyumba hiyo imepata hitilafu ya umeme na kuanza kuungua.

Mashuhuda wa ajali hiyo wamesema walipoona moshi mkubwa unatoka kwenye nyumba hiyo mida ya saa 4:15 usiku walijaribu kwenda kuvunja na kuwaokoa watu waliokuwa kwenye nyumba hiyo na kuwakuta kwenye hali mbaya hivyo walifanya jituhada za kuwafikisha hospitali lakini majibu baadae yalitoka kuwa wamefariki wote watano.