*********************************
“Mwalimu Nyerere alisema Deni la kukata miti bila kupanda ni Deni haramu.unawaibia ambao hawajazaliwa.kwa hiyo yeye alijua umuhimu wa kuhifadhi hii misitu na yeye atabaki kuwa kielelezo bora cha Uhifadhi kutokana na mchango wake Kiula.
Nao Wadau wa Misitu na Utalii kupitia vipindi vya Wanawake kutoka Jiji la Dar es salaam kikiwemo kikundi cha CODECO,Wanawake na Mafanikio na Wanawake Wazalendo kwanza, wameeleza jinsi wanavyofurahia uwepo wa Hifadhi za Misitu Asilia ambayo imekuwa fursa muhimu ya watu kufanya utalii wa ndani.
“Tunashukuru TFS kwa kuandaa hii siku ya kumbukizi ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere , tumemuenzi kwenye kitu alichokipenda sana, alipenda Misitu iwepo ndiyo maana tumeweza kuja kutalii. Hii ni Fursa ya kila mtanzania kufanya Utalii wa ndani “Veradiana Nsongo, Mratibu Msaidizi CODECO.
Naye Maria Mapunda ambaye ni kiongozi wa Kikundi cha Wanawake na Mafanikio ameshukuru TFS kwa kuipa thamani siku ya kumbukizi ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na kuandaa utaratibu wa kufanya utalii katika Vivutio mbalimbali vya Utalii vinavyopatikana katika Hifadhi ya Msitu wa Mazingira asilia Pugu.