wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi akizungumza na makundi mbalimbali ya
vijana waliohudhuria katika Kongamano la Kumbukizi ya Baba wa Taifa, Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere kwenye eneo la Chuo cha Uhasibu mkoani hapa.
RC Nchimbi akikabidhi zawadi ya Rozari Takatifu kwa vijana waliohudhuria
Kongamano la Kumbukizi ya Mwalimu Nyerere kwenye Chuo cha Uhasibu mkoani hapa, kama
ishara ya heshima kwa mama huyo wa Yesu, ambaye Waumini wa Kanisa Katoliki na
marafiki wa karibu hupata fursa ya kumkumbuka kwa kusali rozari
kila ifikapo mwezi Mei na Oktoba kila mwaka.
Mratibu
wa Kongamano hilo na Afisa wa Vijana kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Frederick
Ndahani akizungumza na vijana wa mkoa huo kabla ya kumkaribisha RC Nchimbi
kufungua kongamano.
wa Vijana Omary Mwangi, akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt Rehema Nchimbi
zawadi ya Kitabu cha Historia ya Mwalimu Nyerere.
mkoani hapo wakimkabidhi mama Nchimbi picha ya Mwalimu Nyerere iliyochorwa kwa
umahiri mkubwa na vijana wa mkoa.
Washiriki wakisikiliza kwa makini nasaha za Mkuu wa Mkoa
(hayupo pichani)
Washiriki wakisikiliza kwa makini nasaha za Mkuu wa Mkoa
(hayupo pichani)
Washiriki
wakisikiliza kwa makini nasaha za Mkuu wa Mkoa (hayupo pichani)
wa Wawezeshaji wa Kongamano hilo, Jacob Kanka akitoa mada .
Godwin Myovela na Dotto Mwaibale, Singida
MKUU wa Mkoa wa Singida Dk. Rehema Nchimbi amewataka vijana
kuanza kufikiri ‘sawa-sawa- katika muktadha wa kuongozwa na tafakuri ya kina
kujua na kuona sawa-sawa historia ya taifa la Tanzania lilipotoka, lilipo na
linapoelekea.
Alisema kama vijana watafikiri sawasawa ni lazima watakuwa
na upeo mkubwa wa jicho la kuona sawasawa mnyororo mzima wa hatua kadhaa za
kimaendeleo zilizofikiwa hatua kwa hatua tangu uhuru
Nchimbi alitoa nasaha hizo wakati akizungumza na vijana
mbalimbali jana, kupitia ‘Kongamano la
Kumbukizi ya Baba wa Taifa 2020, lililofanyika jana kwenye Chuo cha Uhasibu
mkoani hapa
“Tusipofanya tafakuri ya kina hata tafsiri ya vitu
vinavyofanywa na serikali hatutaviona, na matokeo yake itakuwa ni rahisi sana
kudanganywa na wapotoshaji wasiolitakia mema taifa letu,” alisema Nchimbi na
kuongeza: “Kijana ukifikiri sawasawa utaona sawasawa, utatekeleza sawasawa na
utaamua sawasawa.”
Mkuu wa Mkoa aliwaambia vijana kuwa bila ya kumfahamu vizuri
na kumtazama Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kamwe hawawezi kuwa kiunganishi
mahiri kwenye mnyororo wa kiuchumi kutoka kwenye Uchumi wa Kati kwa sasa,
kuelekea uchumi wa Juu wa Kati
“Vijana ndio watendaji, na kumbukeni miradi yote hii mikubwa
ya kitaifa inayotekelezwa na serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na kipenzi
chetu Rais John Pombe Joseph Magufuli inafanyika kwa fedha zetu za ndani na zaidi
ni kwa manufaa yenu vijana…fikirini sawasawa ili muone sawasawa,” alisema
Mama Nchimbi alisema Tanzania ni urithi wetu tulioachiwa na
Baba wa Taifa, hakuna urithi mwingine, hivyo vijana wanapomkumbuka wana jukumu
la kumuenzi kwa kusimama vizuri, kuwa na uzalendo na kujifunza historia ya
nchi, ili hatimaye kwenda kwa kasi na tija inayodhihirika katika kulifikisha
Taifa kwenye uchumi wa juu wa kati
“Kijana huwezi kujiangalia wewe bila ya kumtazama Baba wa
Taifa…Nyerere ni alama muhimu sana, ili tushiriki ipasavyo kwenye uchumi huu wa
kati ni lazima tuijue historia ya tulipotoka kati ni dhahiri tutakuwa na
majawabu ya je…hatua hii ya uchumi wa kati, amani na uhuru vinaamanisha nini?..na
ni lazima twende katika fikra zitakazotuonyesha sisi ni taifa la Tanzania na
sio vinginevyo,” alisema Nchimbi.
Awali, Mratibu wa Kongamano la Kumbukizi ya Baba wa Taifa
2020, Frederick Ndahani, alisema Mwalimu Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema “Mjenga
nchi ni Mwananchi na Mvunja nchi ni Mwananchi” hivyo kama vijana wanathamini
sana amani, na kamwe hawatavunja miiko wala kutumika na yeyote kwa maslahi yake
binafsi, kuvuruga amani na utulivu uliopo.
“Sisi vijana wa mkoa huu tumeshuhudia maono ya Baba wa Taifa
yakiwa yanatekelezwa kwa kasi katika serikali hii ya Awamu ya Tano kwenye
Elimu, Afya, Maji, Kilimo, Madini, Mawasiliano, Miundombinu, Nishati na miradi
mingine mingi…hii inatupa taswira na matumaini makubwa kama vijana katika
mustakabali wa maisha yetu kwa sasa na vizazi vijavyo,” alisema Ndahani.
Ndahani ambaye ni Afisa Vijana wa Mkoa, na mmoja wa vijana
shupavu waliokimbiza Mwenge wa Uhuru nchi nzima kwa mwaka 2017, alisema kama
vijana wanajivunia na kutambua mchango mkubwa wa maendeleo katika sekta
mbalimbali, uliofanywa na viongozi wa Taifa la Tanzania kuanzia Mwalimu Nyerere
mpaka sasa chini Rais John Magufuli.
“Tunawashukuru sana viongozi wetu kwa maono na hatimaye kutufikisha
kwenye uchumi huu wa kati. Na kipekee kwa niaba ya vijana wa mkoa huu
namshukuru sana Rais Magufuli kwa busara na hekima za alizojaliwa Mwenyezi
Mungu kwa namna alivyofanikiwa kulivusha salama taifa hili dhidi ya janga
hatari la Corona,” alisema Ndahani na kuongeza:
“Miongoni mwa wahanga wakubwa wa gonjwa hili tulikuwa ni
sisi vijana, lakini leo hii kwa ushupavu na ujasiri wa Rais Magufuli
tunaendelea kama kawaida na masomo yetu kwenye shule na vyuo vyote nchi nzima,
lakini pia tunaendelea kujiachia kwa kukusanyika kama hivi leo…katika kujadili
na kukumbushana majukumu yetu kama vijana kwa mustakabali chanya wa Taifa
letu,” alisisitiza Ndahani.