Home Siasa Sillo azidi kupepea Babati vijijini kumuombea Kura Magufuli.

Sillo azidi kupepea Babati vijijini kumuombea Kura Magufuli.

0

**********************************

Na John Walter-Babati

Mbunge mteule wa Babati vijijini Daniel Baran Sillo ameendelea na kampeni za kunadi ilani ya uchaguzi ya chama cha Mapinduzi (Ccm) ya mwaka  2020-2025, na kumuombea kura Mgombea Urais John Pombe Magufuli na waombea nafasi ya udiwani.

Mbunge huyo anaesubiri kuapishwa ili kuanza kuwasemea wananchi wa Jimbo la Babati vijijini katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amewaomba wananchi wamchague Rais  Magufuli aendelee kuongoza nchi.
Amesema Chama cha Mapinduzi kikiongozwa na mafiga matatu kuanzia Diwani, Mbunge na Rais itakuwa rahisi kufanya shughuli za kuwaletea wananchi maendeleo.
Akizungumza na wananchi katika kata za Magara na Nkaiti tarafa ya Mbugwe, amesema Mgogoro uliopo kati ya wafugaji wanaoishi jirani na hifadhi ya Jamii WMA, atazungumza na wataalamu ili kuwekwa mipaka ambayo itawezesha kutambua mwisho wa Wafugaji na mwekezaji.
Amesema ili kuweza  kutatua changamoto mbalimbali katika jimbo hilo wananchi wamchague Rais Magufuli na madiwani wote wa Chama cha Mapinduzi.
Naye Katibu wa Jumuiya ya wazazi Ccm wilaya ya Babati vijijini Hassan Kim, amewaomba wananchi waendelee kukiamini chama hicho na kuepuka kuchagua kiongozi kwa kuangalia mirungi ya dini, ukabila na ukanda.
Katika ziara hiyo ya Kampeni, Mbunge huyo mteule Daniel Sillo anatoa nafasi kwa wananchi kueleza changamoto walizonazo.
Jimbo la Babati Vijijini linalipatikana mkoa wa Manyara lina jumla ya vijiji 102 ambapo kabla ya uchaguzi mkuu Oktoba 28,2020 Mbunge huyo anatakiwa awe amehitimisha ziara ya Kampeni.