Home Mchanganyiko MAGUFULI APOKEA GAWIO LA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 100 KUTOKA BARRICK

MAGUFULI APOKEA GAWIO LA ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 100 KUTOKA BARRICK

0

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli akiwahutubia Watanzania katika Hafla ya kupokea gawio la Tsh.Bilioni 100, kutoka kwa Kampuni ya Madini ya Twiga Mineral na Shirika na Madini la Taifa (STAMICO), iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli, akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya dola za Kimarekani Milioni 40, kutoka kwa kampuni ya madini ya Twiga Minerals katika hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam, wengine ni Msajili wa Hazina, Athumani Mbutuka, Waziri wa Fedha na Mipango, Philip Mpango, Watendaji wa Shirika hilo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James.Waziri wa Fedha na Mapingo, Dkt.Philip Mpango (wa pili kulia), akishuhudia utoaji wa gawio kwa mfano wa hundi yenye thamani ya dola za Kimarekani Milioni 40, kutoka kwa kampuni ya madini ya Twiga Minerals katika hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam, kulia kwake ni Msajili wa Hazina, Athumani Mbutuka na watendaji kutoka Kampuni hiyo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli, akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya  dola za Kimarekani Milioni 40, kutoka kwa kampuni ya madini ya Twiga Minerals katika hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam, kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Doto James, Watendaji Wakuu wa wa Kampuni ya Twiga Minerals Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Philip Mpango na  Msajili wa Hazina, Athumani Mbutuka. Mwenyekiti wa Bodi STAMICO, Meja Jenerali(Mst), Michael Isamuhyo na Wakuu wa Shirika hilo wakionyesha mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi bilioni 100 mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli (hayupo pichani),  katika hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli, akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi bilioni 100 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi STAMICO, Meja Jenerali(Mst), Michael Isamuhyo, katika hafla iliyofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC), Jijini Dar es Salaam.

*****************************************

Na Beatrice Sanga & Lilian Shembilu-MAELEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amepokea gawio la zaidi ya shilingi bilioni 100 kutoka kampuni ya madini ya Twiga inayomilikiwa kwa ubia kati ya Serikali ya Tanzania na kampuni ya Barrick Gold Mining.

Hafla hiyo imefanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julisu Nyerere(JNICC), Jijini Dar es Salaam,  ampapo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, viongozi wa dini pamoja na wadau mbalimbali wa sekta ya madini nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo Rais Magufuli ameipongeza kampuni ya Barrick kwa kukubali kukaa chini na kufanya mazungumzo na serikali ya Tanzania yaliyopelekea kuanzishwa kwa kampuni ya Twiga Mineral Company ambayo imepelekea kuleta mafanikio kwa Watanzania ambao walikuwa hawafaidiki na madini wanayochimba.

“Napenda niwashukuru Barrick kwanza kwa kukubali kufanya mazungumzo na serikali, ninawashukuru sana kwa sababu mazungumzo yale yalichukua zaidi ya miaka miwili, wapo watu waliobeza sana na mpaka leo bado wapo na walikuwa ni Watanzania na ndio maana nasema Barrick ahsanteni sana” amesema Rais Magufuli

Ameongeza, kuwa  soko la madini nchini Tanzania limeongezeka kwa kiwango kikubwa  ambapo mwaka 2019 mapato yaliyokuwa yanatokana na madini yalikuwa hayazidi bilioni 268 lakini sasa mapato yanayotokana na madini yanafika bilioni 528.  Hii imetokana na jitihada mbalimbali ambazo serikali ya Awamu ya Tano imezifanya ili kuboresha  mifumo ya upatikanaji na uuzaji wa madini zikiwemo kuboresha  sheria ya madini ambayo imepelekea  wachimbaji wadogo na wakubwa kunufaika.

Rais Magufuli amebainisha kuwa sekta ya madini imetengeneza zaidi ya ajira milioni 1 kwa Watanzania lakini pia serikali ya Awamu ya Tano imeweza kutoa mafunzo kwa wachimbaji  zaidi ya 10,000  na kuimarisha taasisi ya geology nchini  ambapo imepelekea kukua kwa sekta ya madini.

Aidha Rais Magufuli  ametoa wito kwa Watanzania  na wasio Watanzania, wakiwemo viongozi wa dini pamoja na waserikali kuwekeza katika sekta ya madini ili waweze kufaidika na madini yaliyopo Tanzania,  waweze kukua kiuchumi na kukuza uchumi wa Tanzania kwa ujumla na kuweza kuongeza kiwango cha mabilionea.

“Napenda nichukue fursa hii kuendelea kuwakaribisha wawekezaji ndani na nje ya nchi kuwekeza hapa nchini, serikali ninayoiongoza haiwachukii wawekezaji ila ina wapenda wawekezaji na ndio maana tuliingia kwenye makubaliano na kampuni ya kimataifa ya Barrick. Anaetaka kuwekeza anakaribishwa sana.” amesema Magufuli.

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Madini Mheshimiwa  Doto Biteko amempongeza na kumshukuru Mhe.Rais Magufuli kwa jitihada alizofanya na kuweza kuibadilisha sekta ya madini  na kufanya wachimbaji wa madini wawe na uhakika wa soko, zaidi kwa kuifanya Tanzania kuwa kituo kikuu cha kuuza madini

“Mheshimiwa Rais sekta hii ya madini imebadilika sana na kama kuna mtu mmoja aliyeibadilisha sekta hii ni wewe, mambo yote yanayotokea kwenye sekta hii yasingeweza kutokea kama kusingekuwa na utashi na msukumo mkubwa ambao umekuwa ukifanya toka ulivyoingia madarakani na kwa michakato mbalimbali ambayo wewe mwenyewe umeisimamia na ambayo umekuwa ukitupa mar azote pale wizarani tunakushukuru sana Mhe.Rais na Mungu akubariki sana” amesema Mhe.Biteko.