Home Mchanganyiko BENJAMINI MKAPA KINARA UTOAJI WA HUDUMA BORA ZA AFYA NCHINI IKIADHIMISHA MIAKA...

BENJAMINI MKAPA KINARA UTOAJI WA HUDUMA BORA ZA AFYA NCHINI IKIADHIMISHA MIAKA MITANO TANGU KUANZISHWA KWAKE

0

Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa Dkt.Alphonse Chandika,akiwalisha Keki Mkurugenzi wa utawala Hospitali ya Benjamini Mkapa Bi.Neema Tawale ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 5 tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo leo jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa Dkt.Alphonse Chandika,akiwalisha Keki wateja waliofika katika hospitali hiyo kupata huduma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 5 tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo leo jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa Dkt.Alphonse Chandika,akiwalisha Keki watumishi wa hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 5 tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo leo jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa Dkt.Alphonse Chandika,akiwalisha Keki Mfanyakazi wa Hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 5 tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo leo jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa Dkt.Alphonse Chandika,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea mafanikio yaliyopatika katika hosptili hiyo ndani ya miaka mitano  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo leo jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa Dkt.Alphonse Chandika,akisisitiza jambo kwa  waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea mafanikio yaliyopatika katika hosptili hiyo ndani ya miaka mitano  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo leo jijini Dodoma.

Baadhi ya watumishi pamoja na waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa Dkt.Alphonse Chandika (hayupo pichani ) wakati  akielezea mafanikio yaliyopatika katika hosptili hiyo ndani ya miaka mitano  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo leo jijini Dodoma.

Daktari Bingwa wa magonjwa ya kinamama na uzazi katika hospitali ya Benjamini Mkapa  Dk Januarius Hinju,akielezea jinsi walivyotoka na walipo kwa miaka mitano wamepata mafanikio makubwa na kuwa sehemu ya mafanikio hayo  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa hospitali hiyo leo jijini Dodoma

Muuguzi wa Hospitali ya Benjamini Mkapa,Debora Mwobasa,ambaye ni muuguzi wa mwanzo wakati Hospitali inaanza akielezea mafanikio yaliyopatikana ndani ya miaka mitano ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka mitano tangu Hospitali hiyo ianzishwe.

…………………………………………………………………………………

NaAlex Sonna,Dodoma.

Hospitali ya Benjamini Mkapa Jijini Dodoma imefanikiwa kufanya upandikizaji wa  figo kwa wagonjwa 13 Nchini kwa kipindi cha miaka mitano na kuendelea kuwa kinara  katika utoaji wa huduma bora za afya.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamini Mkapa Dkt.  Alphonce Chandika wakati akizungumza na waandishi wa habari katika kuadhimisha miaka mitano  tangu kuanzishwa kwa Hospitali hiyo mwaka 2015 amesema kuwa imekuwa na mafanikio ambayo yamechangiwa na serikali kuimarisha uwekezaji  katika vifaa tiba vya kutolea  huduma kwa wananchi.

“Mwaka 2018 kwa kushirikiana na wadau wengine wakiwemo watu kutoka nchini Japan tulianza huduma ya upandikizaji wa figo hivyo tangu kuanza kwa hospitali hiyo tumeshapandikiza figo wagonjwa 13 na hayo ni mafanikio makubwa kuna hospitali zina zaidi ya miaka 50 hazijawahi kufanya hivyo kwa hiyo tusiwategegemee sana watu wa njeamesema

Dk Chandika ameongeza kuwa wakati hospitali hiyo inazinduliwa ilikuwa na changamoto ya kuazima  wahudumu wa afya wa 22 lakini hadi sasa imefanikiwa kuwa na watumishi 456.

Wakizungumzia mafanikio ya hospitali hiyo kwa kipindi cha miaka mitano Mkurungezi kitengo cha upasuaji Dk Januarius Hinju pamoja na Muuguzi ,Debora Mwobasa wamebainisha kuwa wamefanya kazi kwa juhudi kubwa ili kuwasaidia wananchi licha ya kuanza utoaji wa huduma kwa changamoto mbalimbali mwaka 2015.

“Kwa kweli tunashukuru kwa hospitali ya Benjamin Mkapa kwa juhudi kubwa hizi nasi kama wataalm wa Afya tumekuwa bega kwa bega kufanya juhudi kubwa na kwa ufanisi katika hospitali hii”

Nao baadhi ya wanachi jijini Dodoma wameipongeza hospitali hiyo kwa kutoa huduma sitahiki kwa jamii kwa kipindi cha miaka 5.

Hospitali hii ya Benjamin Mkapa, ilianzishwa mwaka 2015 kwa tamko la Rais wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Dkt.  Jakaya Mrisho Kikwete na ilizinduliwa rasmi Oktoba 13  ya Mwaka huo.