Home Siasa DKT. BASHIRU AWAOMBA WATANZANIA KUTOFANYA MAJARIBIO YA UONGOZI

DKT. BASHIRU AWAOMBA WATANZANIA KUTOFANYA MAJARIBIO YA UONGOZI

0

………………………………………………………………………………………

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally, amewaomba watanzania kutofanya majaribio ya uongozi wa nchi kama baadhi ya vyama vinavyoendelea kuwalaghai kwa kuomba kujaribiwa.

Ameyasema hayo tarehe 10 Oktoba, 2020 katika mkutano wa kampeni jimbo la Ukonga.

“Hakuna Chama kingine mpaka leo tunapozungumza chenye uzoefu na uwezo wa kulinda umoja, upendo na mshikamano wa Taifa hili isipokuwa CCM.”

“Ndugu zangu, ninawaomba tusiwajaribu watu wasio na uzoefu, CCM inaouzoefu, inaweza kuwa na upungufu fulani kwa kuwa ni Chama cha watu sio cha malaika, lakini katika eneo la kulinda uhuru, Usalama, amani, umoja, mshikamano wa kitaifa na muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Hakuna Chama kingine cha kukupa uhakika katika hayo isipokuwa CCM.”

Wakati huo huo, Katibu Mkuu ameongeza kuwa, Chuki, ghasia na vurugu zikishamiri hazichagui Chama, zitaathiri kila mmoja, hivyo ni muhimu wananchi wanapokwenda kupiga kura kutazama kwa makini ni Chama kipi kinaweza kuwahakikishia usalama wao, na mpaka sasa CCM imedhihirisha inao uwezo huo kwa vitendo.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu ameendelea kusisitiza msimamo wa Chama na Mgombea Urais wa CCM Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli wa kuendelea kuwajibu kwa hoja wapinzani licha ya wao kutumia matusi na kejeli, na dawa yao ni kutokuwapa kura za Udiwani, Ubunge na Urais.