Home Michezo BURUNDI YALIPA KISASI KWA TAIFA STARS,YAICHAPA 1-0 MECHI YA KIRAFIKI UWANJA WA...

BURUNDI YALIPA KISASI KWA TAIFA STARS,YAICHAPA 1-0 MECHI YA KIRAFIKI UWANJA WA MKAPA

0

Na.John Bukuku,Dar es Salaam

Timu ya Burundi (Intamba Murugamba) imelipa kisasi kwa Taifa Star kwa kuichapa bao 1-0 katika Mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki kwenye uwanja wa  Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

Ushindi wa Burundi ni kulipa kisasi baada ya kuondoshwa na Tanzania katika kuwania Michuano ya CHAN.

Timu zote zilianza kipindi cha kwanza kwa kushambuliana kwa zamu huku zikikosa nafasi ya kupata bao hadi mapumziko hakuna aliyekuwa na bao.

Kipindi cha pili timu zote zilianza kwa mabadiliko huku dakika za mwanzo Tanzania ilipoteza nafasi mbili za kupata bao baada ya Simon Msuva na Shomar Kapombe kukosa nafasi za wasi.

Tanzania ilipata pigo dakika ya 76 kwa kiungo wake Mkabaji Jonas Mkude kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kuchezeana rafu na mwamuzi kumuonyesha kadi ya pili ya njano na kuwa Nyekundu.

Baada ya kupata kadi Nyekundu Burundi waliliandama lango la Tanzania kama nyuki huku Kipa David Mapigano akiokoa michomo hatari.

Juhudi za Burundi zilizaa matunda dakika ya 85 Saidi Ntibazonkiza akiwanyanyua mashabiki wake kwa bao la shuti kali lililomshinda Mlinda mlango David Mapigano akiruka bila mafanikio yoyote.

Hadi dakika 90 Mwamuzi Martin Sanya akimaliza Mpira wenyeji wametoka kichwa chini kwa kutandikwa bao 1-0 na Intamba Murugamba.