Home Siasa KATIBU UWT DODOMA MJINI AWAOMBA WANAWAKE KATA YA IHUMWA WASIFANYE MAKOSA OKTOBA...

KATIBU UWT DODOMA MJINI AWAOMBA WANAWAKE KATA YA IHUMWA WASIFANYE MAKOSA OKTOBA 28,2020

0

Na.Alex Sonna,Dodoma
Mmefurika,tangu nianze ziara za kusaka kura za CCM toka Moyoni mwangu wanawake wa Ihumwa Shikamonii! hiyo ni sauti ya mpambanaji akiwa na kamati yake ya ushindi  Katibu wa Umoja wa Wanawake wa CCM Wilaya ya Dodoma Mjini, Diana Madukwa ameshangazwa na mapokezi ya wanawake katika Kata ya Ihumwa akiwa na kwenye ziara ya Kata kwa Kata akisaka kura.
Madukwa akizungumza kwenye Mkutano wa wanawake wa Kata ya Ihumwa  amewaomba   wanawake wote wa kata  hiyo kuhakikisha wanazitafuta kura nyingi za wagombea wa chama cha mapinduzi ili waweze kushinda kwa kishindo.
”Kwa jinsi nilivyowaona kwa mapokezi yenu naamini hamtaniagusha kwa kura wito wangu kila aliyepo hapa akatafute kura kwa watu 30 kila mmoja na siku ya uchaguzi muwapitie ili kata hii muweze kuongoza kwa kura za kishindo”amesema Madukwa
Hiki ni kikao cha ndani wanawake wa Kata ya Ihumwa naombeni kura zenu kwa wingi kwa wagombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, Mgombea Ubunge Jimbo la Dodoma Mjini, Anthony Mavunde na madiwani wote wa Kata 41 ziwe za kishindo.
Madukwa amesema miaka mitano ya Dk Magufuli imekuwa ya heshima sana kwa Dodoma kwani licha ya kuihamishia serikali hapa lakini pia kitendo cha kuipa Dodoma hadhi ya Jiji kumeongeza fursa kubwa za kimaendeleo.
Amesema miaka mitano ya Dk Magufuli imeshuhudia Jiji hilo likiongoza kwa mapato, likiongoza kwa mtandao wa lami nchini kwa kuwa na Km 129 pamoja na kuletewa miradi mikubwa ya kimkakati ikiwemo Stendi ya kisasa, Soko kubwa Afrika Mashariki pamoja na eneo la mapumziko la Chinangali.
” Niwaombe akina Mama Msidanganyike  na wapinzani, nimepata taarifa wanapita kwenu kuwalaghai muwape vitambulisho vya kupigia kura, msijaribu kufanya hivyo kwani mtapoteza haki yenu ya msingi, msidanganywe na maneno yenu hawana uwezo wa kuongoza kwa sababu vyama vyao wenyewe tu vinawashinda, mambo yaliyofanywa na Dk Magufuli kwa miaka mitano kiongozi mwingine angeyafanya kwa miaka 20, tusimuangushe twendeni tukampe kura nyingi za kishindo.
Wapinzani wanachohubiri wao ni maandamano tu, sasa ndugu zangu sisi tunataka kuandamana au tunataka maendeleo? Hawana hata ilani ya Uchaguzi, sisi tukija tunasema tumejenga vituo vya afya 480, tumejenga hositali ya Wilaya 71, tumekarabati shule kongwe, tumetoa elimu bure, wao wakija watasema nini? Tusihadaike Oktoba 28 tukamchague Magufuli,” Amesema Madukwa.
Hivyo nawaomba wanawake mjitokeze  kwa wingi Oktoba 28 mkiwa na vitambulisho vyenu vya mpiga kura ili Muweze kumchagua mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, Mbunge wa Jimbo hilo Anthony Mavunde na madiwani wote wa kata 41 za Dodoma Mjini.