Home Siasa January Makamba asema Bumbuli wanajambo lao kwa Magufuli ahidi watampa...

January Makamba asema Bumbuli wanajambo lao kwa Magufuli ahidi watampa tisini kwa tisini

0

**********************************

Katibu Mstaafu wa SUKI na Mbunge Mteule wa Jimbo la Bumbuli January Makamba ametoa ahadi ya kuvunja rekodi ya kumchagua Mgombea wa CCM ngazi ya Urais, John Magufuli kwa kumpa asilimia 90 ya ushindi katika uchaguzi utakaofanyika October 28 mwaka huu.

Makamba alitoa Kauli hiyo jana Mbele ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati kuu ya CCM Taifa Kassim Majaliwa wakati alipopita kuwasalimia wakazi wa bumbuli na kuomba kura za Magufuli na Madiwani wa chama cha mapinduzi.

“Bumbuli tunajambo letu October 28 ambalo tumelipa jina la tisini kwa tisini yaani tunakuahidi Waziri Mkuu tutavunja rekodi ya kumchagua Magufuli” Alisema Makamba

Makamba alieleza kuwa Mwaka 2015 kwa jimbo la bumbuli walimchagua Rais Magufuli kwa asilimia 86 lakini Mwaka huu wa uchaguzi wamejipanga kuvunja rekodi ya kumchagua kwa asilimia 90 sababu amewajali wakazi wa jimbo hilo kwa kuwapelekea miradi ya maendeleo.

Makamba ambaye kwasasa anasubiri kuapishwa kuwa Mbunge wa Jimbo hilo alisisistiza kuwa Wanachagua Rais ambaye atakuwa Amir Jeshi Mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama ambaye atakayeamuru majeshi yetu kwenda vitani hivyo ni lazima kutazama hulka ,busara na malezi yake kisiasa na ukoo wake kisiasa ambapo Alisema ukoo wa Magufuli ni CCM.

Alieleza kuwa CCM imekuwa na historia ya kutoa maamiri jeshi tangu uhuru nakwamba wapinzani wao hawajawahi kujaribiwa kutoa mtu ambaye ataamuru ata Wanamgambo.

Makamba ambaye ni Katibu Mstaafu wa Suki alisema tunapochagua Rais hatuchagui mtu mdogo nakwamba Wanachagua mtu ambaye anaweza kuamuru nchi kwenda kwenye vita wakati wowote hivyo aliwataka wananchi wawemakini katika kuchagua.

” Watazameni wale wengine wanapozungumza,wapohutubia ,wasikilizeni kauli zao arafu tujiulize wanastahili kuamuru majeshi yetu? Jamani mtu pekee tuyeweza kumkabidhi majeshi yetu na tukalala kwa amani ni Magufuli pekee”Alisema January Makamba.

Aliongeza kuwa mnachagua mtu ambaye ni kielelezo na taswira ya nchi yetu duniani nakwamba wakimpeleka huko ulimwenguni maneno atakayozungumza yatakuwa na tafsiri ya Tanzania ni nchi ya namna gani hivyo katika wagombea wote wa upinzani hakuna ata mmoja ukimuweka kwenye mimbari ukasema huyu ataiwakilisha vyemaTanzania tukajisikia fahari zaidi ya magufuli.