Home Michezo KOCHA KMC FC ATOLEA UFAFANUZI WA KICHAPO CHA MECHI MBILI MFULULIZO

KOCHA KMC FC ATOLEA UFAFANUZI WA KICHAPO CHA MECHI MBILI MFULULIZO

0

Mara baada ya kupoteza mchezo wa mzunguko wa tano dhidi ya Polisi Tanzania, Kocha wa Timu ya Manispaa ya Kinondoni KMC FC Habibu Kondo amesema kuwa bado anakiamini kikosi hicho kutokana na uwezo waliokuwa nao wachezaji wake.

 Kocha Habibu ametoa kauli hiyo leo wakati Timu ya KMC FC ilipokuwa ikifanya  mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo unaofuata dhidi ya Cost Union mchezo utakaopigwa Oktoba 14 Katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Kocha Habibu amesema kuwa kupitia mazoezi hayo timu hiyo inajiandaa kikamilifu katika kujiweka tayari dhidi ya mchezo huo na kwamba makosa yaliyofanywa na wachezaji hao katika mchezo uliopita yanafanyiwa kazi.
Habibu amefafanua kuwa anakiamini kikosi hicho kwakuwa kinauwezo mzuri  kikubwa kwasasa ni kuendelea kujenga utulivu kwenye nafasi za kumalizia ili kupata matokeo mazuri katika mchezo huo unaofuata.
 “Timu inatengeneza nafasi nzuri kwenye michezo lakini kwenye umaliziaji inakuwa changamoto,  kupitia mazoezi haya tunakwenda kukisuka kikosi chetu ili kwenye michezo ijayo tupate matokeo ambayo awali tulikuwa tukiyapata” amesema Kocha Habibu.