Home Siasa DK. TULIA AWAUMBUA WAPINZANI MBELE YA WAPIGA KURA MBEYA “WANATOROKA”

DK. TULIA AWAUMBUA WAPINZANI MBELE YA WAPIGA KURA MBEYA “WANATOROKA”

0

…………………………………………………………………………….

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya CCM Dr. Tulia Ackson amefanya kampeni katika kata ya Nonde jijini humo akiwaomba Wananchi wakipigie kura za kishindo chama chake katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika October 28, 2020 huku akieleza baadhi ya mambo aliyokwisha wafanyia wakazi wa Nonde pamoja na yale atakayowafanyia endapo watampa ridhaa ya kuwatumikia kwa kipindi cha miaka mitano.

“Ninaposema huu ni muda wa hesabu namaanisha kwamba tunataka kujua mtu anayetaka kuomba kura hapa atueleze ameshafanya nini kabla ya kuja, sasa mimi leo nitawapa mifano michache tu, nilipofika hapa shule ya msingi Nonde nilielezwa baadhi ya changamoto ikiwemo ya miundombinu na nikaleta mifuko ya Cement nyinyi wenyewe ni mashahidi.”- Dr. Tulia Ackson

“Sasa kwanini mshindwe kumchagua Tulia amekupa baadhi ya mifano ambayo amekwishaanza kufanya jambo kuliko anayetaka kuja kuwaomba kura wakati hakuna alichowafanyia. Ndugu zangu chagueni Tulia Mama wa Connection niwafanyie mambo maana yote tuliyoyafanya ni mwanzo tu shughuli bado haijaanza, chagueni Chama Cha Mapinduzi kuanzia Rais, Mbunge na Madiwani mjionee mvua ya kazi hapa”- Dr. Tulia Ackson

“Chagua Mbunge mwenye Connection na Rais ambaye ana hela, nasikia watu wanasema oooh! Serikali awamu ya tano imewekeza kwenye miundombinu ya vitu na sio watu mbona wao wamewekeza kwenye ujenzi wa hoteli kwani hayo ni maendeleo ya nini? Watu wanashangaza sana na safari hii hawa wote tunasukuma nje..”-Dr. Tulia Ackson

“Ndugu zangu Nonde safari hii tunachagua Tulia anayetulia Bungeni sasa ukichagua mbunge ambaye kila siku anatoroka Bungeni imekula kwetu, ukichagua Mbunge ambaye mjadala ukiletwa Bungeni yeye anajiziba mdomo na kutoka nje hapo imekula kwetu. Mbunge ni muwakilishi wa Wananchi lazima aende akatusemee na sio kukimbia sasa dawa yake safari hii kwa pamoja tunaenda na Tulia”-Dr. Tulia Ackson