Home Biashara BENKI YA TPB SHINYANGA YAENDELEA KUSHEREHEKEA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

BENKI YA TPB SHINYANGA YAENDELEA KUSHEREHEKEA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA

0

Askofu Zakayo Bugota wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (A.I.C.T) Dayosisi ya Shinyanga akikata keki maalumu kwa ajili ya wateja wa Benki ya TPB.
 
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Benki ya TPB tawi la Shinyanga inaendelea kusherehekea Wiki ya Huduma kwa Wateja iliyoanza Jumatatu Oktoba 5,2020 ambapo leo Oktoba 7,2020, Wafanyakazi wa Benki ya TPB wamekata keki maalumu kwa ajili ya wateja wa Benki ya TPB na kunywa chai ya pamoja na wateja wa TPB Bank wakiongozwa na Askofu Zakayo Bugota wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (A.I.C.T) Dayosisi ya Shinyanga.
 
Meneja wa Benki ya TPB Tawi la Shinyanga Julius Mataso ametumia fursa hiyo kuwashukuru na kuwapongeza wateja wa TPB Bank kwa kuendelea kuiamini na kutumia huduma za Benki ya TPB ikiwemo kutuma fedha ndani na nje ya nchi na mikopo mbalimbali huku akiwaahidi kuwa Benki ya TPB itaendelea kuboresha zaidi huduma zake.
 
 ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Meneja wa Benki ya TPB Tawi la Shinyanga Julius Mataso akiwashukuru na kuwapongeza wateja wa TPB Bank kwa kuendelea kuiamini na kutumia huduma za Benki ya TPB leo Jumatano Oktoba 7,2020 wakati wafanyakazi wa Benki ya TPB wakinywa chai na wateja wa benki ya TPB. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Wateja wa Benki ya TPB wakiwa ndani ya Benki ya TPB Tawi la Shinyanga

 

Muonekano wa Keki Maalum zilizoandaliwa na Benki ya TPB tawi la Shinyanga kwa ajili ya Wateja wa Benki ya TPB katika  maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.

 

Askofu Zakayo Bugota wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (A.I.C.T) Dayosisi ya Shinyanga akikata keki maalumu kwa ajili ya wateja wa Benki ya TPB.
Mfanyakazi wa Benki ya TPB Grace Gemu akikata vipande vya keki baada ya Askofu Zakayo Bugota wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (A.I.C.T) Dayosisi ya Shinyanga akikata keki maalumu kwa ajili ya wateja wa Benki ya TPB.
Meneja wa Benki ya TPB Tawi la Shinyanga Julius Mataso akimlisha keki mteja wa Benki ya TPB, Askofu Zakayo Bugota wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (A.I.C.T) Dayosisi ya Shinyanga
Meneja wa Benki ya TPB Tawi la Shinyanga Julius Mataso akimlisha keki mteja wa Benki ya TPB
Meneja wa Benki ya TPB Tawi la Shinyanga Julius Mataso akimlisha keki mteja wa Benki ya TPB
Meneja wa Benki ya TPB Tawi la Shinyanga Julius Mataso akimlisha keki mteja wa Benki ya TPB
Meneja wa Benki ya TPB Tawi la Shinyanga Julius Mataso (wa tatu kushoto) na wafanyakazi wa Benki ya TPB wakigawa vitafunwa na chai kwa wateja wa Benki ya TPB  ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja
Askofu Zakayo Bugota wa Kanisa la African Inland Church Tanzania (A.I.C.T) Dayosisi ya Shinyanga akichukua vitafunwa na chai ndani ya Benki ya TPB
Meneja wa Benki ya TPB Tawi la Shinyanga Julius Mataso  akiongoza wafanyakazi wa Benki ya TPB kuchukua chai
Wafanyakazi wa Benki ya TPB wakichukua chai
Wafanyakazi wa Benki ya TPB wakichukua chai
Wafanyakazi wa TPB Bank na Wateja wakiendelea kunywa chai
Wafanyakazi wa TPB Bank na Wateja wakiendelea kunywa chai
Meneja wa Benki ya TPB Tawi la Shinyanga Julius Mataso,  wafanyakazi wa Benki ya TPB na Wateja wa Benki ya TPB wakipiga picha ya pamoja baada kula keki na kunywa chai ya pamoja ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja katika benki hiyo.
 
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog