Home Siasa SHIGONGO AENDELEA KUCHANJA MBUGA VIJIJI VYA BUCHOSA

SHIGONGO AENDELEA KUCHANJA MBUGA VIJIJI VYA BUCHOSA

0

****************************************

LICHA ya ratiba ya kampeni ya mgombea ubunge Jimbo la Buchosa kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Eric Shigongo James, kuwa ngumu, mgombea huyo ametembelea ujenzi wa zahanati ya Kijiji cha Kasheka, Kata ya Bagwe, iliyojengwa kwa nguvu za wananchi na kujionea hali ambapo imefikia hatua ya kuezekwa.

Akikagua zahati hiyo, Shigongo amesema moja ya kazi atakazozifanya endapo atachaguliwa ni kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa ikiwa ni pamoja na ujenzi wa zahanati kila kijiji ambao ni mpango wa serikali na kuhakikisha zinafanya kazi ya kuwahudumia wananchi.

Aidha, amewapongeza wananchi wa Kasheka kwa kuthubutu na kutumia nguvu zao wenyewe kujenga majengo ya zahanati hiyo huku akiwasisitiza kuendelea kujitolea, jambo ambalo litasaidia kuharakisha maendeleo ya mtu binafsi na jamii ya Kasheka kwa jumla.

Si ujenzi wa zahanati tu, bali amewaeleza wananchi wa Buchosa kuwa atashirikiana nao hata kuchimba mashimo ya vyoo vya shule ili wafanunzi wasihangaike kujisaidia vichakani.

Shigongo anaendelea na kampeni zake jimboni Buchosa akinadi sera za chama chake cha CCM pamoja kuwaomba ridhaa wananchi ili wawachague viongozi wa CCM kuanzia kiti cha urais, ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu.

NA IDD MUMBA | GPL