Home Siasa KATIBU UWT WILAYA YA DODOMA AZIDI KUCHANJA MBUGA KUSAKA KURA ZA CCM...

KATIBU UWT WILAYA YA DODOMA AZIDI KUCHANJA MBUGA KUSAKA KURA ZA CCM KATA KWA KATA

0

Katibu wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT), Wilaya ya Dodoma, Diana Madukwa (katikati) akiwa wanawake wa Kata ya Mbabala wakiimba wimbo mara baada ya kufanya ziara ya kusaka kura za kishindo kwa mgombea urais wa chama cha mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli,Mbunge pamoja na madiwani wa kata 41  ili chama hicho kiendelee kushika dola.

Katibu wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT), Wilaya ya Dodoma, Diana Madukwa (katikati) akisaini kitabu mara baada ya kuwasili katika  Kata ya Mbabala wakati wa ziara ya kuongea na wanawake wa kata hiyo akitafuta kura za mgombea urais wa chama cha mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli,Mbunge pamoja na madiwani wa kata 41  ili chama hicho kiendelee kushika dola.

Katibu wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT), Wilaya ya Dodoma, Diana Madukwa akizungumza na wanawake wa Kata ya Mbabala akiendelea kutafuta kura Kata kwa Kata kwa mgombea urais wa chama cha mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli,Mbunge pamoja na madiwani wa kata 41  ili chama hicho kiendelee kushika dola.

Katibu wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT), Wilaya ya Dodoma, Diana Madukwa akimuombea kura mgombea udiwani Kata ya Mbabala Pascazia Mayala wakati wa kikao cha ndani na  wanawake wa Kata ya Mbabala alipokuwa akiendelea na kutafuta kura Kata kwa Kata kwa mgombea urais wa chama cha mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli,Mbunge pamoja na madiwani wa kata 41  ili chama hicho kiendelee kushika dola.

Sehemu ya wanawake wa Kata ya Mbabala wakionyesha mabango yakiwa na Picha ya Mgombea Urais wa ccm Dkt.Magufuli kwa Katibu wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT), Wilaya ya Dodoma, Diana Madukwa (hayupo pichani ) alipofanya ziara ya kusaka kura Kata kwa Kata kwa wagombea wa chama cha mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli,Mbunge pamoja na madiwani wa kata 41  ili chama hicho kiendelee kushika dola.

Mjumbe wa Halmashauri Wilaya ya Dodoma ambaye pia ni Mumbe wa Kamati ya Ushindi Bi.Romana Nyoni,akiongea na wanawake wa Kata ya Mbabala wakati wa kikao cha ndani cha kusaka kura Kata kwa Kata chenye lengo la kupata ushindi wa kishindo kwa wagombea wa CCM.

Mjumbe wa Halmashauri Wilaya ya Dodoma ambaye pia ni Mumbe wa Kamati ya Ushindi Bi.Romana Nyoni,akipiga magoti kwa wanawake wa Kata ya Mbabala akiomba kura kwa mgombea udiwani wa Kata hiyo Pascazia Mayala wakati wa kikao cha ndani cha kusaka kura Kata kwa Kata chenye lengo la kupata ushindi wa kishindo kwa wagombea wa CCM.

Mgombea udiwani wa Kata ya Mbabala Pascazia Mayala ,akiomba kura kwa wanawake wa Kata hiyo wakati wa ziara ya Katibu wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT), Wilaya ya Dodoma, Diana Madukwa wa kutafuta kura Kata kwa Kata

Wanawake wa Kata ya Mbabala wakiendelea kufatilia Mkutano wa ndani wakati wa ziara ya Katibu wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT), Wilaya ya Dodoma, Diana Madukwa akiendelea kuchanja mbuga kusaka kura za CCM Kata kwa Kata.

………………………………………………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

Katibu wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi(UWT), Wilaya ya Dodoma, Diana Madukwa,ameendelea na ziara ya kutafuta  kura za chama cha mapinduzi (CCM) kata kwa kata kwa lengo la kuhakikisha wanapata kura nyingi za mgombea urais wa chama cha mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli,Mbunge pamoja na madiwani wa kata 41  ili chama hicho kiendelee kushika dola.

Akizungumza kwenye Mkutano wa wanawake wa Kata ya Mbabala,amewaomba   wanawake wote wa kata  hiyo kuhakikisha wanazitafuta kura nyingi za wagombea wa chama cha mapinduzi ili waweze kushinda kwa kishindo.

Madukwa amesema kuwa Rais Dk. Magufuli amefanikiwa kuboresha sekta ya elimu kwa kutoa elimu bure,kukarabati majengo ya shule na kujenga majengo mapya mengi na amefuta michango shuleni hivyo wanawake wa Wilaya ya Dodoma mnapaswa kumtafutia kura Dk. John pombe Magufuli,Mavunde pamoja na diwani wetu Pascazia Mayala

” Dodoma sisi tumefaidika sana na Dk Magufuli kwanza ametuheshimisha kwa kuleta Makao Makuu ya Nchi hapa, wizara zote na taasisi ziko Dodoma hii ni fursa kubwa sana kwetu, ametujengea soko na stendi kubwa ambayo itakuwa chanzo cha mapato kwa Jiji letu, niwaombe Oktoba 28 mjitokeze kwa wingi mkapige kura”amesema Madukwa

Hivyo nawaomba wanawake mjitokeze  kwa wingi Oktoba 28 mkiwa na vitambulisho vyenu vya mpiga kura ili Muweze kumchagua mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, Mbunge wa Jimbo hilo Anthony Mavunde na madiwani wote wa kata 41 za Dodoma Mjini.

Aidha Madukwa amewaomba wanawake wa Kata ya Mbabala  kutumia ushawishi wao kuhakikisha wanampigia kura nyingi mgombea huyo wa chama cha mapinduzi Dk.John pombe Magufuli kwa kuwa anauwezo wa kuliongoza taifa hili kimaendeleo kuliko wagombea wengine.

Madukwa amesema kwa miaka mitano ya Dk Magufuli wanawake wamenufaika na mikopo ya serikali inayotolewa kwenye Halmashauri zote nchini ambayo imekuwa haina riba wala makato yoyote jambo ambalo limewafanya kina mama wengi kupiga hatua za kimaendeleo.
Dodoma ya leo siyo kama ya zamani, miaka mitano nyuma tulikuwa hatuna barabara za lami tulizonazo leo, Dk Magufuli amepambana na changamoto zetu kwa kiasi kikubwa na amefanikiwa, tusimvunje moyo, tukampe kura nyingi za kishindo,” Amesema Madukwa.
Hata hivyo Madukwa amewataka wanawake hao kutokubali kutoa vitambulisho vyao vya kupigia kura kwa watu wanaopita kwenye maeneo yao wakiahidi kuwapatia mikopo.

Madukwa amaesema kuwa kuna watu wameanza kupita wanachukua vitambulisho hivyo wakiahidi kuwapatia mikopo jambo ambalo si kweli kwa kuwa wamekuwa wakichukua na kwenda kutengeneza nakala inayofanana na kitambulisho hicho.

“Hawa wanachukua na kwenda kutoa ‘copy’ ambayo inakuwa ngumu kama kitambulisho, siku ya kwenda kupiga kura unakuta tayari ulishapiga kura kumbe hujapiga, ndugu zangu msikubali kuwapa watu hao wanaokusanya vitambulisho kitambulisho ni haki yako wewe kwa hiyo nawakumbusha mkatunze vitambulisho vyenu,”amesema Madukwa

Awali Mjumbe wa Halmashauri Wilaya ya Dodoma ambaye pia ni Mumbe wa Kamati ya Ushindi Bi.Romana Nyoni,amewataka wanawake kumchagua Diwani wa Kata ya Mbabala Pascazia Mayala kwa sababu ni mwanamke anayejua uchungu wa maendeleo ya kata hii.
”Wanawake wenzangu nawaomba nawapigia magoti nendeni mkatafute kura za Dk.Magufuli,Mavunde na Mayala tumieni lugha ya ushawishi mkiwa ndani kwa akina baba ili tuweze kushinda kwa kushindo”amesema Bi.Nyoni.
Bi.Nyoni amewahimiza wanawake wa Kata hiyo kuchagua Mgombea wa Urais,ubunge na udiwani kwa kuwa hao ndio wanaweza kuleta maendeleo ya kweli kwa wananchi wa kat hii.

Kwa upande wake, Mgombea udiwani kata ya Mbabala,Pascazia Mayala  amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili kutimiza haki yao ya kimsingi na kuchagua viongozi bora wa CCM.

“Tukampe heshima Rais wetu Magufuli kama alivyotupa heshima wanadodoma, tumpe heshima Mbunge wetu Mavunde ili afanye kazi aliyobakisha, na Mimi pia mnipe kura nyingi za kutosha niwatumikie wana Mbabala, nawaahidi tutakuwa bega kwa bega kuleta maendeleo kwa kata yetu,”amesema Mayala