Home Mchanganyiko BILIONI 13 ZATEGWA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI VIJIJINI  MKOANI GEITA

BILIONI 13 ZATEGWA KUTEKELEZA MIRADI YA MAJI VIJIJINI  MKOANI GEITA

0

Timu ya wataalam ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Prosper Buchafwe wakipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Hamza Guni wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Geita (GEUWASA) kuhusu uboreshaji wa huduma ya maji Kata ya Kasamwa mjini Geita.

Timu ya wataalam wakikagua tenki la maji la Nyampa lenye ujazo wa lita elfu 60 katika mradi wa uboreshaji huduma ya maji katika kata ya Kasamwa.

Wananchi wa kata ya Kasamwa wakipata huduma ya majisafi na salama baada ya uboreshaji wa huduma ya maji katika kata yao.

Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Maji Bw. Prosper Buchafwe akimsikiliza kwa makini Meneja wa RUWASA Halmashauri ya Wilaya ya Chato Mhandisi Endrew Kilembe kuhusu utekelezaji wa mradi wa maji wa Imalabupina Inchwankima wenye thamani ya shilingi bilioni 8.2.

………………………………………………………………………………………

Wananchi wa vijijini mkoani Geita watanufaika na huduma ya majisafi kutoka asilimia 60 hadi kufikia asilimia 75 ifikapo mwezi Desemba, 2020 baada ya kiasi cha shilingi bilioni 13 kupangwa kukamilisha miradi ya maji.

Meneja wa Wakala wa Usambazaji Majisafi na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) mkoa wa Geita Mhandisi Nicas Ligombi amesema miradi hiyo ya maji utekelezaji wake upo katika hatua mbalimbali za ujenzi kati ya asilimia 70 mpaka asilimia 80 ili kukamilika. 

“Hakika tunategemea ifikapo Desemba, 2020 kukamilisha miradi yote na kiwango cha upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama katika maeneo ya vijijini kwa mkoa wa Geita kitaongezeka kutoka asilimia 60 hadi kufikia asilimia 75”, Mhandisi Nicas Ligombi amesema.

Naye, Meneja wa RUWASA wa wilaya ya Chato Mhandisi Andrew Kilembe amesema utekelezaji wa mradi wa maji wa Imalabupina Inchwankima umefika asilimia 90 katika ujenzi wa miundombinu ya maji na vijiji vitano kati ya 11 vinavyotakiwa kunufaika na mradi huo tayari vinapata huduma ya maji. Vijiji hivyo vinavyopata huduma ya maji ni Nyamirembe, Kalebezo, Nyambiti, Busalala na Imalabupina

Amesema mradi huo ukikamilika wananchi zaidi ya elfu 59 watanufaika na huduma ya majisafi na salama katika vijiji vya, Nyamirembe, Kalebezo, Nyambiti, Busalala Imalabupina, Inchwankima, Kachwamba, Ipandikilo, Idoselo, Mwangaza na Igalula 

Mhandisi Kilembe amesema hadi sasa mradi umefikia na asilimia 100 kwa upande wa ununuzi wa mabomba na fedha zilizokwishalipwa kwa wakandarasi M. M. Industries na Ndeenengo Senguo Co. Ltd ni kiasi cha shilingi bilioni 7.2. 

Wakati huo huo, Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Maji Bw. Prosper Buchafwe amewaelekeza watendaji hao wa RUWASA mkoani Geita kuongeza juhudi zaidi za usimamizi wa miradi ya maji ili wananchi wapate huduma hiyo mapema. 

MAELEZO YA PICHA

  1. Timu ya wataalam ikiongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bw. Prosper Buchafwe wakipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Hamza Guni wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Geita (GEUWASA) kuhusu uboreshaji wa huduma ya maji Kata ya Kasamwa mjini Geita. 
  2. Timu ya wataalam wakikagua tenki la maji la Nyampa lenye ujazo wa lita elfu 60 katika mradi wa uboreshaji huduma ya maji katika kata ya Kasamwa.
  3. Wananchi wa kata ya Kasamwa wakipata huduma ya majisafi na salama baada ya uboreshaji wa huduma ya maji katika kata yao.
  4. Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Maji Bw. Prosper Buchafwe akimsikiliza kwa makini Meneja wa RUWASA Halmashauri ya Wilaya ya Chato Mhandisi Endrew Kilembe kuhusu utekelezaji wa mradi wa maji wa Imalabupina Inchwankima wenye thamani ya shilingi bilioni 8.2.