Home Mchanganyiko WANACHAMA WA MAGROUP YA WHATSAPP SHINYANGA ‘SHY TOWN VIP’ WAFANYA SHEREHE KUBWA...

WANACHAMA WA MAGROUP YA WHATSAPP SHINYANGA ‘SHY TOWN VIP’ WAFANYA SHEREHE KUBWA …KATAMBI AWAFAGILIA

0

Muonekano keki maalumu kwa ajili ya wanachama wa Magroup ya Whatsapp Shinyanga ‘SHY TOWN VIP’ iliyotengenezwa na Mariam Cake kwa ajili ya sherehe ya wanachama wa magroup ya Whatsapp Shinyanga ‘SHY TOWN VIP PARTY’
 
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog 
Haijawahi kutokea!! Ndivyo unavyoweza kusema. Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania wanachama ‘Members’ wa Makundi ya Mtandao wa Kijamii ‘Magroup ya Whatsapp’ mkoani Shinyanga kupitia Group maarufu kwa jina la ‘SHY TOWN VIP’ wamefanya sherehe kubwa iliyowakutanisha pamoja ili kufahamiana uso kwa uso,kula pamoja na kupata burudani. 
 
Sherehe hiyo iliyopewa jina la ‘SHY TOWN VIP PARTY’ imefanyika usiku wa Jumamosi Oktoba 3,2020 katika Ukumbi wa Starehe/Burudani wa La Prince Pub mjini Shinyanga na kukutanisha pamoja watumiaji wa mtandao wa kijamii Whatsapp waliopo katika magroup takribani 8 ya Whatsapp Shinyanga likiwemo Group Maarufu kwa jina la ‘SHY TOWN VIP’. 
 
Sherehe hiyo ambayo mchana Oktoba 3,2020 ilitanguliwa na shughuli ya wanachama hao wa Magroup ya Whatsapp waliochangishana fedha na vitu mbalimbali kufanikisha sherehe kutembelea kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu cha Buhangija Mjini Shinyanga na kuwapatia zawadi kadha wa kadha imehudhuriwa pia na Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia CCM,Patrobasi Katambi ambaye pia ni mmoja wa wanachama wa Magroup ya Whatsapp ya Shinyanga. 
 
Sherehe hizo pia zimenogeshwa na Burudani kutoka kwa vikundi vya burudani na wasanii mbalimbali kutoka mkoa wa Shinyanga akiwemo Patrick Alsina aliyekuwa mshiriki shindano la BSS,Nyumbu Mjanja, Nyassani, Hans Q, Kundi la Kambi ya Nyani na The Fighters. 
 
Akizungumza wakati wa kufungua sherehe hiyo, Mgeni Rasmi ambaye alikuwa ni Mkurugenzi wa Hilbat School, Dr. Clemence Batisilio amesema magroup hayo ya Whatsapp yamekuwa msaada mkubwa kwa wanachama ambao kupitia magroup hayo wamekuwa wakishiriana kwenye shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kuchangiana pale mwanachama anapopata matatizo. 
 
“Mimi ni mmoja wa wanachama wa Kundi la SHY TOWN VIP,nawapongeza sana kwa umoja huu tunaoendelea nao na hatimaye leo tumekutana Live ili kufahamiana,kula,kunywa na kufurahi pamoja”,alisema. 
 
Aidha aliahidi kuchangia shilingi Milioni 1 kwa ajili ya kununua vifaa vya kutambulisha wanachama wa Group la SHY TOWN VIP ikiwemo sare za wanachama. 
 
Akisoma Risala kwa niaba ya wanachama, Mkurugenzi wa Kampuni ya Lulekia, Bi. Ansila Benedict alisema Group la Shy Town VIP liliasisiwa na MC ICE mwaka 2017 na kwamba sherehe hiyo ni sehemu ya Utambulisho rasmi wa Umoja wa Mtandao wa Whatsapp utakaojulikana kwa jina la ‘SHY TOWN VIP’ akieleza kuwa mipango iliyopo ni kuanzisha SACCOS. 
 
Kwa upande, Patrobas Katambi  ambaye ni miongoni mwa wanachama wa Magroup ya Whatsapp Shinyanga na Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) amewapongeza Wana Shinyanga kwa ubunifu huo mkubwa wa kuwakutanisha pamoja watumiaji wa mitandao ya kijamii akieleza kuwa wameonesha mfano bora nchini na haijawahi tokea popote nchini. 
 
“Natumia nafasi hii kuwapongeza sana kwa ubunifu huu. Nimefurahi sana kwa jambo hili jema mlilolitengeneza. Shinyanga mmefanya kitu cha pekee sana nchini, kinachotakiwa kuwa mfano hata kwenye maeneo mengine nchini .Nami nitajitahidi nashirikiana nanyi ili kuhakikisha kuwa tunatumia mitandao ya jamii kwa ajili ya kujiletea maendeleo”,alisema Katambi. 
 
“Hongereni sana SHY TOWN VIP mkawe mfano wa kuigwa maeneo mengine Tanzania kwani mnatumia Whatsapp kwa mambo ya maendeleo, mnasaidiana katika shida na raha kupitia Magroup ya Whatsapp na kujadiliana masuala kadha wa kadha. Niwapongeze sana pia kwa kutumia siku ya leo kutoa misaada kwa watoto wenye uhitaji pale Buhangija,mmeonesha kiasi gani mnajali utu”,aliongeza Katambi. 
 
Mpiga Picha Mkuu wa Malunde 1 blog,Kadama Malunde ambaye pia ni Mwanachama wa Makundi mbalimbali ya Whatsap Shinyanga,ametuletea picha za matukio yaliyojiri wakati wa Sherehe ya ‘SHY TOWN VIP’. 
 
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mgeni Rasmi ,Mkurugenzi wa Hilbat School, Dr. Clemence Batisilio (mwenye nguo ya bluu) akifungua rasmi sherehe ya wanachama wa magroup ya Whatsapp Shinyanga ‘SHY TOWN VIP PARTY’ iliyofanyika usiku wa Oktoba 3,2020 katika ukumbi wa La Prince Pub Mjini Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog   
Mwanachama wa Magroup ya Whatsapp Shinyanga, Patrobas Katambi na Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) akizungumza kwenye sherehe ya wanachama wa magroup ya Whatsapp Shinyanga ‘SHY TOWN VIP PARTY’ iliyofanyika usiku wa Oktoba 3,2020 katika ukumbi wa La Prince Pub Mjini Shinyanga.
Admin wa Group la SHY TOWN VIP, Raymond Mponda akizungumza kwenye SHY TOWN VIP PARTY
Admin wa Group la SHY TOWN VIP, Orgenes Charles akizungumza kwenye SHY TOWN VIP PARY, Kulia ni MC Zeze ‘ Zezema Shilungushela’ ambaye ndiyo huwa anapokea michango mbalimbali ya wanachama wa SHY TOWN VIP pale mwanachama anapopatwa na tatizo/shida mfano misiba.

Mkurugenzi wa La Prince Pub ambaye ni miongoni mwa viongozi wa magroup ya Whatsapp Shinyanga akizungumza kwenye sherehe ya wanachama wa magroup ya Whatsapp Shinyanga ‘SHY TOWN VIP PARTY’ iliyofanyika usiku wa Oktoba 3,2020 katika ukumbi wa La Prince Pub Mjini Shinyanga. 

Kushoto ni Mkurugenzi wa La Prince Pub, Athanas William akimtambulisha Mkurugenzi wa Malunde 1 blog, Kadama Malunde ambaye pia ni Mwanachama na Mwanzilishi wa Magroup ya Whatsapp Shinyanga

Meneja Masoko wa Kampuni ya Vinywaji TBL ,Shinyanga,Katavi na Tabora, Peter Marijani ambaye ni mwanachama kwenye Magroup ya Whatsapp akizungumza kwenye sherehe ya wanachama wa magroup ya Whatsapp Shinyanga ‘SHY TOWN VIP PARTY’ iliyofanyika usiku wa Oktoba 3,2020 katika ukumbi wa La Prince Pub Mjini Shinyanga. 
Mgeni Rasmi ,Mkurugenzi wa Hilbat School, Dr. Clemence Batisilio (mwenye nguo ya bluu katikati) akikata keki maalumu kwa ajili ya wanachama wa Magroup ya Whatsapp Shinyanga ‘SHY TOWN VIP’ kwenye sherehe ya wanachama wa magroup ya Whatsapp Shinyanga ‘SHY TOWN VIP PARTY’ iliyofanyika usiku wa Oktoba 3,2020 katika ukumbi wa La Prince Pub Mjini Shinyanga. 
Mgeni Rasmi ,Mkurugenzi wa Hilbat School, Dr. Clemence Batisilio (mwenye nguo ya bluu katikati) akikata keki maalumu kwa ajili ya wanachama wa Magroup ya Whatsapp Shinyanga ‘SHY TOWN VIP’ kwenye sherehe ya wanachama wa magroup ya Whatsapp Shinyanga ‘SHY TOWN VIP PARTY’ iliyofanyika usiku wa Oktoba 3,2020 katika ukumbi wa La Prince Pub Mjini Shinyanga. 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Lulekia, Ansila Benedict akimlisha keki Mgeni Rasmi ,Mkurugenzi wa Hilbat School, Dr. Clemence Batisilio.
Mgeni Rasmi ,Mkurugenzi wa Hilbat School, Dr. Clemence Batisilio akimlisha keki Toffee Uptown
Mgeni Rasmi ,Mkurugenzi wa Hilbat School, Dr. Clemence Batisilio akimlisha keki Mwanachama wa Magroup ya Whatsapp Shinyanga, Patrobas Katambi na Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM)
Viongozi wa Magroup ya Whatsapp Shinyanga wakiwa katika meza na Mwanachama wa Magroup ya Whatsapp Shinyanga, Patrobas Katambi na Mgombea Ubunge Jimbo la Shinyanga Mjini (CCM) 
Msanii Nyassani akitoa burudani kwenye sherehe ya wanachama wa magroup ya Whatsapp Shinyanga ‘SHY TOWN VIP PARTY’ iliyofanyika usiku wa Oktoba 3,2020 katika ukumbi wa La Prince Pub Mjini Shinyanga. 
Msanii Patrick Alsina akitoa burudani kwenye SHY TOWN VIP PARTY
Mc Zeze ‘ Zezema Shilungushela’ akizungumza kwenye sherehe ya wanachama wa magroup ya Whatsapp Shinyanga ‘SHY TOWN VIP PARTY’ iliyofanyika usiku wa Oktoba 3,2020 katika ukumbi wa La Prince Pub Mjini Shinyanga. 
MC ICE akionesha makeke yake kwenye sherehe ya wanachama wa magroup ya Whatsapp Shinyanga ‘SHY TOWN VIP PARTY’ iliyofanyika usiku wa Oktoba 3,2020 katika ukumbi wa La Prince Pub Mjini Shinyanga. 
Msanii Nyumbu Mjanja akitoa burudani kwenye sherehe ya wanachama wa magroup ya Whatsapp Shinyanga ‘SHY TOWN VIP PARTY’ iliyofanyika usiku wa Oktoba 3,2020 katika ukumbi wa La Prince Pub Mjini Shinyanga. 
Vijana kutoka Kundi la Kambi ya Nyani wakitoa burudani
Tofee, kundi la Kambi ya Nyani na The Fighters wakitoa burudani
Jikoni mambo yalikuwa motoo!! Nyama choma kwa wingi!!