Home Biashara RC KILIMANJARO AWATAKA WANAWAKE KUPAMBANIA FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA BIASHARA

RC KILIMANJARO AWATAKA WANAWAKE KUPAMBANIA FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA BIASHARA

0
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira akizungumza wakati wa ufunguzi wa kongamano  la kimataifa la wanawake wajasiriamali lililofanyika mjini hapa.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira akizungumza na wanawake wajasiriamali wakati alipotembelea banda la mmoja wa wajasiriamali waliokuwa wakionyesha bidhaa  zao jijini Arusha 
Wanawake wajasiriamali kutoka ndani na nje ya nchi wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano wa wajasiriamali wanawake uliofanyika mjini hapa.(Happy Lazaro).
………………………………………………………………………….
Happy Lazaro,Arusha.
Mkuu wa  Mkoa wa Kilimanjaro  Anna Mghwira  amewataka wanawake kupambania fursa za uwekezaji katika biashara zao kwani  wamekuwa  na mchango mkubwa  Sana katika kuinua uchumi wa  nchi.
Ameyasema hayo Jana wakati akifungua kongamano kubwa la kimataifa la wanawake wajasiriamali kutoka nchi mbalimbali barani ulaya na Afrika mashariki.
Mghwira alisema kuwa,wanawake ni jeshi kubwa na wamekuwa wakidhubutu katika kushiriki fursa mbalimbali za maendeleo Jambo ambalo kongamano hilo litawafanya waendelee kujiinua kiuchumi na kuboresha biashara zao.
Amesema kuwa,wanawake wanapaswa kujiongeza katika shughuli zao na kuhakikisha kuwa wanaongezea thamani bidhaa zao ili ziweze kupata soko ndani na nje ya nchi na kuweza kupanua wigo wa biashara zao.
“wanawake wanapaswa kuendelea kupambana katika kujimarisha katika Masoko ya nje kwa lengo la kuzalisha bidhaa zenye ubora na ushindani wa  nje kwani kazi nyingi zinazo zalishwa nchini zina ubora  wa kiwango cha kuuza nje,hivyo ni wajibu wao kuhakikisha kuwa wanakuwa na udhubutu wa kutosha na kuboresha bidhaa zao ili zijulikane kimataifa.
Kwa upande wake Gladness Katega ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Iamwomenprenear LTD,ambaye pia ni Mratibu  wa kongamano hilo amesema kwamba lengo la kuwakutanisha Wanawake hao ni kujijengea  uwezo pamoja na kutambua fursa za kufanya biashara ndani na nje ya nchi  kwa kuwakutanisha wanawake mbalimbali kutoka nchi za nje ambao wamefanikiwa kibiashara.
Katega amesema kuwa, kongamano hilo limelenga kuwafundisha  wanawake namna ya kupambana na Biashara kimataifa na kitaifa na kufikia malengo ya kukuza biashara zao  kwa mtandao  lengo likiwa ni kuhakikisha bidhaa zao zinafikia wateja nje ya Mkoa wa Arusha na sehemu zingine nchini.
Aliongeza kuwa,wanataka kuhakikisha mafunzo watakayopata kwenye kongamano hilo yatawawezesha namna ya kukuza biashara zao na kuweza kupata soko la uhakika ndani na nje ya nchi na kuweza kujulikana kitaifa.
Baadhi wa washiriki wakiongelea Kongamano hilo na namna watakavyo  nufaika Rejea Vivao  walisema kuwa,kitendo Cha kuwakutanisha wanawake hao kimeleta manufaa makubwa Sana kwani wameweza kubadilishana uzoefu na wenzao wa nje ya nchi namna ya kuboresha biashara zao na kuzifanya ziwe za kimataifa zaidi.
 Aliongeza kuwa ,kikubwa zaidi ni kuwa wanategemea kupata mafunzo yatakayo wasaidia kusonga mbele katika biashara zao na kufikia masoko makubwa ya nje hasa  kwa kutumia mitandao.