Home Siasa MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM MHE.DKT.JOHN MAGUFULI AUNGURUMA KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA...

MGOMBEA URAIS KUPITIA CCM MHE.DKT.JOHN MAGUFULI AUNGURUMA KATIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA VISIWANI ZANZIBAR

0

MGOMBEA Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe.John Pombe Magufuli akihutubia katika mkutano wake wa kampenin
uliofanyika katuika Uwanja wa Mnazi mmoja Jijini Zanzibar  na kuwaombea
kura Wananchi wa Zanzibar na kumuombea Kura Mgombea Urais wa Zanzibar
Mhe. Hussein Ali Hassan Mwinyi pamoja na Wabunge, Wawakilishi na
Madiwani wa CCM Zanzibar.(Picha na Ikulu)

RAIS Mstaaf wa Tanzania  Awamu ya Pili Mhe Ali Hassan  Mwinyi 
akisalimiana na Mgombea Urais wa Tanzania ambae pia ni Mwenyekiti wa CCM
Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzxania Mhe. Dkt. John Pombe
Magufuli alipowasili katika Uwanja wa Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar
kuhudhuria Mkutano wa Kampeni wa Mgombea Urais wa Tanzania uliofanyika
leo 3/10/2020.(Picha na Ikulu)

MGOMBEA Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi
MheDkt. John Pombe Magufuli akisakata rumba na Msanii wa muziki wa
Kizazi kipya Zuchu wakati alipopanda jukwaa la wasanii katika uwanja wa
Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar wakati wa mktano wake wa kampeni uliofanyika
leo 3/10/2020.(Picha na Ikulu) MGOMBEA Urais wa Tanzania kwa Tiketi ya CCM Mhe, Dkt.
John Magufuli akilisakata rumba wakati wa mkutano wake wa kampeni
uliofanyika uwanja wa Mnazi Mmoja leo 3/10/2020 na (kushoto kwake)
Mgombea Urais wa Zanzibar Mhe. Hussein Mwinyi na Makamu Mwenyekiti wa
CCM Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein na Viongozi wengine wa CCM
wakijumuika katika kulishata rumba na msani Zuchu.(Picha na Ikulu)

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Zanzibar ambae pia ni Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,.Dk. Ali Mohamed Shein
akisalimiana na Wananchi waliohudhuria mkutano wa kampeni wa Mgombea
Urais wa Tanzania Mhe. John Magufuli uliofanyika Uwanja wa Mnazi Mmoja
Jijini Zanzibar.(Picha na Ikulu)

WANACHAMA wa Cha Cha Mapinduzi Zanzibar wakishangilia
wakati wa mkutano wa kampeni wa Mgombea Urais wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Magufuli (hayupo pichani) akihutubia na kuwaombea Kura Mgombea Urais wa
Zanzibar Mhe Dk. Hussein Mwinyi na Wabunge, Wawakilishi na Madiwa wa
CCM, wakati wa mkutano huo uliofanyika uwanja wa mnazi mmoja Jijini
Zanzibar leo 3/10/2020.(Picha na Ikulu)

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi
Mhe.Dk. Hussein Mwinyi akiwapungia mkono Wananchi  wa Zanzibar alipokuwa
akiwasili katika uwanja wa mnazi mmoja kuhudhuria mkutano wa kampeni  wa
CCM wa Mgombea Urais wa Tanzania Mhe Dkt. John Magufuli leo
3/10/2020.(Picha na Ikulu)

MGOMBEA Urais wa Tanzania ambae pia ni Mwenyekiti wa CCMTaifa
Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akiwasalimia WanaCCM na Wananchi
waliohudhuria mkutano wa Kampeni  uliofanyika katika uwanja wa mpira
Mnazi Mmoja leo 3/10/2020, na Kushoto kwake) Katibu Mkuu wa CCM Taifa
Dkt. Bashiru Ally, wakielekea katika jukwaa kuu la Viongozi.(Picha na
Ikulu) VIONGOZI wa Jukwaa Kuu wakiwa wamesimama wakati wakiitikia dua
ikisomwa na Sheikh Sharif  Abdulraham Muhidin (hayupo pichani) kabla ya
kuaza kwa mkutano wa kampeni wa CCM uliofanyika katika Uwanja wa Mpira
Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar leo 3/10/2020.(Picha na Ikulu)

WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar wakishangilia
wakati wa Mkutano wa Kampeni wa Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya
CCM Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli uliofanyika katika Uwanja wa Mnazi
Mmoja leo 3/10/2020.(Picha na Ikulu)

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar ambae
pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali
Mohamed Shein, akiwahutubia Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakati wa
Mkutano wa Kampeni ya Mgombea Urais wa Tanzania Mhe.Dkt. John Magufuli
uliofanyika katika Uwanja Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar leo
3/10/2020.(Picha na Ikulu)

WAKE wa Viongozi wakifuatilia hutuba ya Mgombea Urais wa
Tanzania Mhe.John Pombe Magufulia akiwahutubia Wanachama wa CCM Zanzibar
katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika Uwanja wa Mnazi Mmoja
Jijini Zanzibar leo 3/10/2020 na kuwaombea Kura Mgombea Urais wa
Zanzibar Mhe. Hussein Mwinyi na Wabunge, Wawakilishi na Madiwani wa CCM
na kujiombea kura yeye mwenyewe  kwa Wananchi.(Picha na Ikulu)

MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya
Chama Cha Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi akihutubia wakati
wa mkutano wa kampeni ya Mgombea Urais wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe
Magufuli uliofanyika katika Uwanja wa Mnazi Mmoja Jijini Zanzibar na
kuwaomba kura Wananchi wa Zanzibar na kumuombea Kura Mgombea Urais wa
Tanzania Mhe.Dkt.John Magufuli na Wagombea Ubunge, Uwakilishi na Udiwani
  wa CCM Zanzibar.(Picha na Ikulu)

*************************************

MWENYEKITI wa CCM, John Pombe Magufuli amesema akipata ridhaa ya wananchi kuendelea na kipindi Chake cha pili cha urais ataendelea kulinda kwa vitendo Muungano na Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Kauli hiyo aliitoa wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa kampeni katika viwanja vya Mnazi mmoja Zanzibar.
Amewakumbusha Wazanzibar faida ya Muungano ikiwa ni pamoja na kushirikiana katika miradi mikubwa ya maendeleo kati ya Zanzibar na Tanzania bara.
Alisema miongoni mwa faida hizo ni pamoja na mkopo wa Sh trilioni 2.3 zilizokopwa na Serijali ya Muungano kwa Zanzibar pekee ndani ya miaka 40.
“Mkinichagulia Dk Mwinyi jambo la muhimu tutakalofabya ni kuhakikisha tunaulida Muungano wa nchi hizi mbili na MapinduI matukufu ya Zanzibar.
Akimzungunzia Dk Mwinyi, Magufuli alisema kuwa anamfahamu  ni kijana makini, mnyenyekevu, mchapa kazi na ni kijana.
Alisema tangu Muungano uanzishwe Marais walioongoza Zanzibar ni ambao walizaliwa kabla ya Muungano, sasa ameletwa aliyezaliwa baada ya Muungano, ambaye anajua mahitaji ya Wazanzibar wa sasa.
“Hivi sasa asilimia 70 wamezaliwa baada ya Muungano anajua nini wanataka au wanahitaji” alisema.
Alisema Dk Mwinyi pia hana tamaa maana akiwa Waziri wa Ulinzi kwa miaka 11, alifanya kazi kwa uadilifu mkubwa.
“Katika miaka yangubmitano  ya mwanzi nilichunguza mawaziri wote nilimkosa anayenifaa kama DkMwinyi, najiuliza mkimchagua nitapata shida ya  kumteua  Waziri wa Ulinzi mwenye kalba kama huyu” alisema Magufuli.
Alisema  anajua kuna suala la mafuta na gesi, nataka niwahakikishie mafuta yatakayopatikana huku ni ya Wazanzibar, sisi tulipata dhahabu kule.Ndiyo maana mnahitaji mtu makini ili rasilimali hii iwe faida kwenu”alisema.
Alisema waliyoyapanga katika Muungano ni kufuata yaliyomo katika ilani, lakini kuwatumikia Watanzania.
“Iwapo mtamchagua nitashirikiana naye kufanya mapinduzi ya kiuchumi, kupambana na umasikini, kutatua changamoto ya ajira, kuna maeneo mengi ya kushirikiana ikiwamo uchumi wa bluu, utalii, kilimo na  ujenzi wa miundombinu” alisema.
Alisema anafahamu Muungano una changamoto ndogo ndogo ambazo watazimaliza, huku akitolea mfani alivyolitatua sakata la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na Zesco ambapo Zanzibar ilikuwa inadaiwa bilioni 22.9. ” Nlilifuta moja kwa moja hilo deni na nikasena hazilipwi kwa sababu Zanzibar ni Tanzania na Tanzania ni Zanzibar. Sikutaka kuwatwisha mzigo ilihali umeme unatoka Tanzania.
Alisema changamoto haziwezi kuwashinda hasa wakimchagulia  Dk Mwinyi kwa sababu ndege wenye mabawa yanayofanana huruka pamoja. “Mimi na Mwinyi tunafanana kwa sababu sisi wote ni CCM. Nina uhakika tutashirikiana vizuri kudumisha Muungano na kuleta mabadiliko katika nchi yetu” alisema.
Alisema wataifanya Zanzibar kuwa kituo (center) cha biashara kutokana na jiografia take ilivyo na kuwapo kwa wafanyabiashara wengi, “Kuna vikwazo vidogo vidogo tutavishughulikia, niwaahidi wafanyabiashara wadogo wadogo tutawabeba”.
Akitoa ufafanuzi kuhusu kuzuiliwa au kuruhusiwa kuvua bahari kuu kwa sababu ni suala la Muungano, Magufuli alisema alipokuwa waziri wa Uvuvi alilipeleka suala hilo bungeni na kufanya makusudi kuiteua makao makuu ya uvuvi yawe Zanzibar, hivyo hakuna atakayeweza kuwazuia hata meli zinazofanya shughuli hiyo zinasajiliwa huko, hivyo katika suala hilo wanaotakiwa kulalamika ni Watanzania Bara.
Magufuli alisema ” Dk Mwinyi ametoa maombi maalumu, nikuahidi nitashirikiana na we we katika kila hatua, lengo ni kuona maendeleo ya Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla.
“Wananchi nawaambia asipotimiza haya anayoyasema kwa kuwa nitakuwa bado Mwenyekiti wa CCM, mje mniulize” alisema Magufuli.
Alisema uchaguzi huu ni muhimu kwa sababu unaamua ama waendelee na Muungano au twasiendelee, kuwachagua wanaotambua mahitaji ya sasa ya Zanzibar au kwa maslai yao binafsi.
Awali akizungumza katika mkutano huo mgombea urais wa Zanzibar, Dk Mwinyi alisema kuwa walizungumza na Magufuli  wakakubaliana  baada ya uchaguzi atawasaidia katika miradi ya maendeleo ikiwamo barabara zinazohitaji kukamilishwa.
Alisema jambo lingine ni kukamilisha sekta ya maji ambayo kwa sasa imefikia silimia 72, umeme asilimia 78.
“Baada ya uchaguzi iwapo nitapata ridhaa nitakulete orodha ya mambo ninayotaka utusaidie ikiwamo kutuongezea umeme kwa sababu tunaingia katika uchumi mkubwa mahitaji ya nishati hiyo yataongezeka, pia utusaidie kukamilisha ujenzi wa hispitali ya rufaa ya kisasa kule Binguni” alisema.