Home Mchanganyiko TAMKO LA THBUB WAKATI WA  MAADHIMISHO YA SIKU YA WAZEE DUNIANI OKTOBA...

TAMKO LA THBUB WAKATI WA  MAADHIMISHO YA SIKU YA WAZEE DUNIANI OKTOBA MOSI, 2020

0

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Mathew Mwaimu (Jaji mst.) akiwaongoza viongozi na watumishi wa Tume leo (Oktoba 2, 2020) katika upimaji wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza (non-communicable diseases). Zoezi la upimaji afya za watumishi ilikuwa sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani.

Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Mhe. Mathew Mwaimu (Jaji mst.) akiongea na vyombo vya habari mjini Dodoma leo (Oktoba 2, 2020) wakati taasisi hiyo ikiadhimisha Siku ya Wazee Duniani kwa kupima afya zao.

Baadhi ya watumishi wa Tume wakisubiri kupima afya zao wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani leo (Oktoba 2, 2020).

Kamishna wa THBUB, Mhe. Amina Twalib Ally alikuwa miongoni mwa viongozi wa Tume walioshiriki zoezi la upimaji wa afya katika maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani.

Watumishi wa Tume wakipokea ushauri kutoka kwa wahudumu wa afya mara baada ya kupima afya zao leo (Oktoba 2, 2020).

****************************************

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inaungana na wadau wote duniani kuadhimisha siku ya wazee duniani yanayofanyika kila ifikapo tarehe Mosi Oktoba ya kila mwaka. Kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu inasema “Familia na Jamii Tuwajibike kuwatunza Wazee.”

Chimbuko la Siku ya Kimataifa ya Wazee linatokana na Tamko la Baraza la Umoja wa Mataifa kupitia Azimio Na. 45/106 la Mwaka 1990 ambalo linazitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Wazee kila ifikapo tarehe 01 Oktoba ya kila  mwaka. Lengo ni kuongeza uelewa wa jamii kuhusu haki na mahitaji ya wazee. Kwa msingi huu, kupitia siku hii jamii hupata fursa ya kutafakari mafanikio, fursa na changamoto ili kuendelea kuboresha hali ya maisha ya wazee.

Kwa mujibu wa takwimu kutoka  Wizara  ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto na kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2012, Tanzania inakadiriwa kuwa na wazee 2,507,568 (Wanawake 1,307,358, Wanaume 1,200,210) sawa na asilimia 5.6 ya wananchi wote.  Kati ya wazee hao asilimia nne (4%) pekee ndio wanaopokea pensheni na asilimia 96% ya wazee hao wanaishi kwa kujitegemea ama kutegemea familia zao ambazo baadhi hazina uwezo wa kuwatunza.

THBUB inapenda kuzipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa hatua mbalimbali walizozichukuwa katika kuimarisha na kulinda haki za wazee nchini. Jitihada hizo ni pamoja na:

 1. Kukomesha mauaji ya wazee;
 2. Kutoa matibabu bure kwa wazee katika zahanati na vituo vya afya;
 • Kuanzisha Dawati la kuratibu huduma za afya kwa wazee katika ngazi ya Wizara na katika Halmashauri;
 1. Halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya kugharimia uanachama wa wazee katika Mfuko wa Afya ya Jamii;
 2. Kuanzisha mchakato wa mfuko wa Afya ya jamii;
 3. Kuanzisha mchakato wa malipo ya pensheni kwa wazee wote;
 • Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kulipa pensheni jamii kwa wazee wote wenye umri  wa miaka 70+;
 • Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuendelea kuhudumia wastaafu na
 1. Mfuko wa TASAF kuendelea kuhudumia kaya masikini zikiwemo kaya za wazee.

Pamoja na jitihada hizo, bado wazee wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo kimsingi huvunja haki zao na hivyo jitihada za makusudi zinapaswa kuchukuliwa ili kurekebisha kasoro hizo. Changamoto hizo ni pamoja na:

 1. Kutokamilika kwa Sheria maalum inayoweka ulinzi na kuzitambua haki za wazee licha ya Sera ya Wazee kukamilika tangu mwaka 2003;
 2. Kukosekana kwa dawa na vifaa tiba katika hospitali na vituo mbalimbali vya afya pote nchini;
 • Umaskini wa kipato miongoni mwa wazee hususani wale ambao hawakuwa katika ajira rasmi;
 1. Kutokamilika kwa mpango wa pensheni jamii (social Pension) kwa wazee na
 2. Baadhi ya wanufaika wa TASAF hawana sifa stahiki huku wanaostahili kunufaika wakiachwa.

Tume inaamini kuwa Serikali  kwa kushirikiana na wananchi na wadau wa haki za binadamu watazifanyia kazi changamoto hizo katika kuhakikisha kuwa wazee wanatunzwa ipasavyo.

Tukiwa katika kipindi cha uchaguzi, Tume inawaomba wananchi wote na wanachama wote wa vyama vya siasa kuheshimu haki za binadamu hususani haki kwa wazee katika kipindi chote  cha kampeni hadi siku ya kupiga kura. Katika siku ya kupiga kura, Tume ya Taifa ya uchaguzi iwape wazee kipaumbele katika vituo vya kupigia kura na kuwapa msaada na usaidizi maalum ili haki na maamuzi ya wazee yakiheshimiwe.

Tume inaisisitiza jamii kwa ujumla kuhakikisha kuwa wazee kote nchini wanatunzwa ipasavyo. Matunzo hayo pamoja na mambo mengine yanajumuisha kupewa ulinzi na usalama wa maisha ya wazee wote, kupatiwa malazi na chakula bora pamoja na kupewa matibabu katika kuhakikisha kuwa afya za wazee hawa zinaimarika.