Home Siasa BILIONI 1.4 ZATENGWA KUKAMILISHA VIFAA TIBA HOSPITALI YA WILAYA ILEMELA 

BILIONI 1.4 ZATENGWA KUKAMILISHA VIFAA TIBA HOSPITALI YA WILAYA ILEMELA 

0

***************************************

Zaidi ya bilioni moja na milioni mia nne zimetengwa kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021 kwaajili ya kununulia vifaa tiba vitakavyotumika katika hospitali ya wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza ili hospitali hiyo iweze kutoa huduma zote muhimu za afya kwa wananchi wa wilaya hiyo.
Hayo yamebainishwa na mgombea wa ubunge jimbo la Ilemela kupitia chama cha mapinduzi CCM Dkt Angeline Mabula wakati akizungumza na maelfu ya wananchi wa Kata ya Sangabuye waliojitokeza kumsikiliza katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Igalagala mapema asubuhi na jioni kuhitimishia katika  viwanja vya shule ya msingi Kabusungu ambapo amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Mhe Dkt John Magufuli imedhamiria kuboresha sekta ya afya kwa kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma hiyo kutoka umbali mfupi  kwa gharama nafuu hivyo kuamua kutenga kiasi hicho cha fedha kwaajili ya kusaidia hospitali hiyo ya wilaya iweze kutoa huduma zote muhimu bila changamoto yeyote ikiwemo ya ukosefu wa vifaa tiba
‘.. Serikali imetenga zaidi ya bilioni 1.4 kwaajili ya vifaa tiba ili kuhakikisha majengo yale ya hospitali ya wilaya yaweze kufanya kazi iliyokusudiwa bila shaka yeyote ..’ Alisema
Aidha Dkt Mabula mbali na kutaja mafanikio ya sekta ya elimu jimboni humo akaongeza kuwa Serikali imejitahidi kupunguza vifo vya mama na mtoto baada ya kuboresha sekta ya utoaji huduma za afya huku akiwaasa wananchi hao kujiunga na Bima ya afya kwa ni Serikali imeshaanza mchakato wa kuanzisha sheria ya bima ya afya
Kwa upande mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ilemela Ndugu Nelson Mesha akafafanua kuwa nchi ya Tanzania imekuwa ikikabiliwa na maadui wakubwa watatu tangu kipindi cha Uhuru ikiwemo Maradhi, Ujinga na Umasikini hivyo chama chake kila mwaka wa uchaguzi kimekuwa kikitunga Ilani yenye mahitaji ya msingi ya wananchi wake kwa msingi wa kuendelea kupambana na maadui hao wakubwa 
Akihitimisha meneja kampeni Kazungu Safari Idebe akasema kuwa wananchi wa Kata hiyo wamekuwa wakikiamini chama cha mapinduzi kwa muda mrefu na hata uchaguzi uliokwisha wananchi hao waliongoza kwa kutoa kura nyingi kwa CCM hivyo kuwaomba waendelee kukiamini CCM na kukupa kura nyingi za ndio