Home Siasa WAZIRI UMMY ATOA AGIZO KWA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI NCHINI

WAZIRI UMMY ATOA AGIZO KWA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI NCHINI

0

MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa
Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akizungumza na wananchi
wa Kata ya Pongwe Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni

MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akimnadi mgombea udiwani wa
Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi wakati wa mkutano wa kampeni
uliofanyika kata ya Pongwe Jijini Tanga

MWENYEKITI wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba akimuombea kura mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu katikati akiwa na
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba wakitembea
kwenye maeneo mbalimbali Pongwe wakati wa kampeni ya mgombea ubunge wa
Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu

MSANII Kasim Mganga akitumbuiza wakati wa kampeni hizo

Umati Mkubwa wa wananachi wakifuatilia kampeni hizo

Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Tanga Lupakisyo Kapenge kulia akiwa na wadau mbalimbali wakifuatilia mkutano huo

WAZIRI
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amewataka
wakurugenzi wa Halmashauri kote nchini kuacha kuwapa wanawake mikopo kiduchu
ambayo haiwezi kuwasogeza mbele kimaendeleo.

Badala
yake amewataka wawape mikopo itakayowawezesha kuwasaidia kufanya shughuli zao ambazo
zinaweza kubadilisha maisha yao na hivyo kujikwamua kiuchumi wao na jamii zao

Ummy
ambaye pia ni Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) aliyasema hayo wakati
akizungumza na wananch wa Kata ya Pongwe Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa
hadhara ambapo alisema katika hili amedhamiri kuhakikisha linafanyiwa kazi.

“Ninajua
Katika hili ninaongea kama Waziri ninayesimamia Maendeleo ya wanawake
ninawataka wakurugenzi kote nchini kuacha kuwapa wanawake mikopo ya laki tano,
laki mbili, milioni moja badala yake wawapeni ya milioni 5, 10 na 20 ili muweze
kufanya shughuli ambazo zinaweza kubadilisha maisha yenu na sio kuwadanganya na
mikopo kiduchu ambayo haiwezi kuwasogeza mbele”Alisema

Alisema
katika ilani ya uchaguzi ya CCM wamehaidi kwamba endapo watakichagua chama cha
Mapinduzi (CCM) na endapo watamchagua wataongeza idadi ya wanawake watakaopata
mikopo bila riba ili waweze kufanya shughuli zao na ujasiriamali.

“Ninawaomba
sana wanawake wa Kata ya Pongwe ninafahamu hapa kwenu kuna vikundi 7 vimepata
mikopo lakini vingi havijapata mikopo ninawaomba sana katika hili mniamini
nitashirikiana na Diwani tuwafikie wanawake wengi zaidi hivyo ninaomba
mnichague suala hili nikalisimamie kikamilifu”Alisema Waziri Ummy.

Katika
ilani hiyo hawajawashau wafanyabiashara na wajasiramali wadogo wadogo huku
akiwaomba wakiamini chama cha Mapinduzi (CCM) wamchague Rais Joh Magufuli na yeye
ili waweze kuweka mazingira mazuri zaidi ya kwa wafanyabsiuara wadogo wadogo,
wajasiramali wadogo wakiwemo mama ntilie wauza ngenge na vijana wa bodaboda
waweze kufanya shughuli zao bila vikwazo.

“Lakini
pia ninatambua hapa Pongwe kuna matatizo ya upatikanaji wa maji bado maeneo ya
Kakindu,Kisimatui na Kilango na hili limeanza kuonekana baada ya maji kupelekwa
Muheza hapa kwetu Pongwe upatikani wa maji umekuwa changamoto niwaombe mniamini
nitalifanyia kazi”Alisema

 

Ummy
alisema kwamba tayari alikwisha kuanza kulifanya kazi suala hilo na Tanga Uwasa
tayari wamekwisha kupata fedha za kuboresha mtandao wa maji  ili kuweza kuongeza idadi ya kaya na nyumba ambazo
zinapata maji safi na salama ili kuhakikisha maji yanapatikana kwenye eneo hilo
kwa muda mrefu.