Home Siasa DKT MABULA: TUMIENI MABARAZA YA WAZEE KUTATUA KERO ZENU.

DKT MABULA: TUMIENI MABARAZA YA WAZEE KUTATUA KERO ZENU.

0
…………………………………………………………….
Mgombea ubunge wa jimbo la Ilemela kupitia chama cha mapinduzi Dkt Angeline Mabula amewataka wazee wanaoishi jimboni humo kutumia fursa ya uwepo wa mabaraza ya wazee kwa ngazi za mitaa, kata hadi wilaya  kwa kuwasilisha kero zao na kuzipatia ufumbuzi.
Rai hiyo ameitoa wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Kawekamo ikiwa ni muendelezo wa mikutano yake ya kampeni kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kwa mara nyingine ya kuongoza wananchi hao ambapo amefafanua hatua zilizochukuliwa na Serikali ya awamu ya tano juu ya kulinda maslahi ya wazee ikiwemo kutoa huduma bure za afya na utoaji wa ruzuku kwa watu wasiojiweza kupitia mpango wa kunusuru kaya masikini maarufu kama TASAF
‘ Tutumie uwepo wa mabaraza ya wazee kwaajili ya kumaliza kero zetu, Serikali ya awamu ya tano ni sikivu imetoa kipaumbele kwa wazee hata kwenye huduma za afya ‘ Alisema
Aidha Dkt Mabula akafafanua kuwa kwa Kata ya Kawekamo miradi mbalimbali ya maendeleo imetekelezwa ikiwemo ujenzi wa madarasa ya shule ya sekondari Kilimani, ujenzi wa vyoo vya kisasa shule ya msingi Pasiansi, utoaji wa mikopo kiasi cha zaidi ya shilingi milioni 62 na urasimishaji wa makazi na umilikishaji hati.
Akimkaribisha mgombea huyo, Meneja kampeni Ndugu Kazungu Safari Idebe akawataka wananchi hao kuwaamini wagombea wa chama cha mapinduzi kwa kuwapigia kura nyingi za ndio ifikapo Oktoba 28 ili iwe rahisi kutekeleza shughuli za maendeleo badala ya kusikiliza porojo za wagombea wasioitakia mema nchi na wapinga maendeleo.
Akihitimisha katibu wa ccm wilaya ya Ilemela Bi Aziza Isimbula akawataka wananchi hao kuchagua wagombea wa CCM kwa nafasi za Urais, Ubunge na Udiwani kwani ni wagombea wenye sifa, malengo na Ilani iliyobeba mustakabali wa maendeleo ya wananchi hao.
Katika mkutano huo wa kampeni baadhi ya wanachama wa vyama pinzani walirudisha kadi zao za uanachama wa vyama hivyo akiwemo  Bwana Vincent Selestine Mambo aliyekuwa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA baada ya kuridhishwa na utekelezaji wa shughuli za maendeleo nchini uliiongozwa na Rais Mhe Dkt John Magufuli