Home Siasa Mauji ya Mwenyekiti wa UVCCM Vyuo na Vyuo Vikuu Iringa Yatikisa Taifa

Mauji ya Mwenyekiti wa UVCCM Vyuo na Vyuo Vikuu Iringa Yatikisa Taifa

0

***************************************

NJOMBE 

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John Pombe Magufuli ametoa salamu ya pole na Ubani wa shilingi mil 5 kwa familia ya mzee Polkap Mlelwa kufuatia kifo cha kijana wake Emmanuel Mlelwa aliyekuwa mwenyekiti wa uvccm vyuo na vyuo vikuu mkoa wa Iringa kuuwawa kikatili septemba 20 na mwili wake kutupwa na watu wasiojulikana.

Akizungumza mbele ya waombolezaji wakati wa kumpumzisha katika nyumba ya milele kijijini Kwao Luvuyo kilichopo kata ya Madope wilayani Ludewa Dr frank Hawasi ambaye ni katibu nec uchumi na fedha ccm taifa amesema punde ya baada ya kusikia mauaji hayo rais Magufuli akampa agizo la kufika nyumbani kwa wafiwa na kutoa ujembe alio mwagiza.

Dr Hawasi ambaye pia ni mlezi wa chama cha mapinduzi mkoa wa Njombe amesema rais ametoa agizo wahusika wote watafutwe walipo na kisha hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Awali Msemaji wa familia Silvanus Msigwa akitoa historia ya marehemu amesema tangu makuzi yake hakuwahi kuwa na makundi na migogoro na wenzie na kwamba taarifa za kifo zimewapa wakati mgumu kama familia.

Kuhusu hatua zilizochukuliwa hadi sasa Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhandisi Marwa Rubirya anasema tayari watuhumiwa 2 wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tukio hilo huku Katibu wa vijana CCM mkoa wa Njombe Amos Kusakula akieleza hisia za umoja wa vijana mkoani humo kuwa limeshitua na kuwasikitisha mno

Kijana Emmanuel Polkap Mlelwa aliyekuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Iringa alikuwa mkoani Njombe likizo na alitoweka tangu septemba 20 hadi mwili wake ulipobainika septemba 26