Home Mchanganyiko WALEMAVU ILALA – TUNAKWENDA NA MAGUFULI

WALEMAVU ILALA – TUNAKWENDA NA MAGUFULI

0

Kuelekea Uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Tarehe 28 October Mwaka huu, Vikundi Mbali Mbali vya Walemavu vilivyopo katika Manispaa ya Ilala Vimeahidi kumchagua Tena Dkt. John Pombe Magufuli ili endelee kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa muhula wa Pili .

Hayo yamezungunzwa Kwa Nyakati Tofauti Mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Ng’wilabuzi ludigija ambaye alifanya Ziara Maalum ya kutembelea Vikundi vya Walemavu Wilayani humo kwa lengo la kufahamu Changamoto zao.

Katika Ziara hiyo Mhe .Ng’wilabuzi ambaye aliambatana na Katibu Tawala wake Ndugu Charangwa Selemani pamoja na Maofisa Maendeleo ya Jamii Kutoka Manispaa ya Ilala, DC huyo aliwasihi Vijana hao kufanya Kazi bila kuogopa kwani Rais Magufuli amewathamini Sana Walemavu kwa kuwawezesha Mikopo isiyo na riba hivyo wao waendelee kuchapa kazi kwa Uhuru na yeye kwa Mamlaka aliyonayo atahakikisha anawatetea kwa kila Hali .

Miongoni mwa Vikundi vulivyotembelewa na DC Ludigija ni Vijana ambao wanamiliki Bajaji zaidi ya 8 baada ya kuwezeshwa Zaidi ya Milioni 40 kikundi kilichopo Ilala Machinga Complex wamesema kuwa Ombi lao Kubwa Ni kuruhusiwa kuingia Katikati ya Jiji bila bughudha kwani kwa Sasa wamekua wakikamatwa Sana bila kujali hali ya ulemavu walonayo ndipo Mh Ludigija alipowaahidi kukufanyia kazi Swala lap Hilo kwa kukutana na Mamlaka za Jiji.