Home Michezo SIMBA YAZIDI KUITAFUTA AZAM FC LIGI KUU,YAICHAPA 3-0 GWAMBINA FC

SIMBA YAZIDI KUITAFUTA AZAM FC LIGI KUU,YAICHAPA 3-0 GWAMBINA FC

0

…………………………………………………………….

Na.Alex Sonna

Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara wekundu wa Msimbazi Simba wamezidi kuongeza kasi kwa  kuitafuta Azam FC katika Msimamo wa Ligi kuu Vodacom  baada ya kuitandika mabao 3-0 timu ya Gwambina FC kutoka Misungwi Mkoani Mwanza katika uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam

Mabao ya Simba yamepatikana kipindi cha kwanza na cha pili yakifungwa na Medie Kagere dk ya 41,Pascal Wawa dk 51,Chris Mugalu

Hii ni mechi ya nne kwa timu ya Gwambina FC wakiwa hawajapata ushindi wowote ule tangu wapande Ligi Kuu licha ya kufungwa  wameonyesha uwezo wa hali ya juu kwa kucheza Mpira mzuri.

Kwa ushindi huo Simba imefikisha Pointi 10 huku ikiwa imecheza mechi nne na kuchupa hadi nafasi ya pili ikizidiwa Pointi mbili na Azam Fc ambao wanaongoza Ligi wakiwa na Pointi 12 wakicheza mechi nne bila kufungwa wala kuruhusu nyavu zao kutikisika,

Ligi Kuu itaendelea kesho kwa Ruvu Shooting kuwa wenyeji wa Biashara United Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam, Mwadui FC na Ihefu Uwanja wa Mwadui Complex, Kishapu mkoani Shinyanga na Mtibwa Sugar na Yanga SC Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.

Raundi ya Nne ya Ligi Kuu itakamilishwa Jumatatu kwa mchezo mmoja tu, Coastal Union wakiwa wenyeji wa JKT Tanzania kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.