Home Siasa Dkt. TULIA ATEMA CHECHE MBEYA “SAFARI HII HATUDANGANYIKI”

Dkt. TULIA ATEMA CHECHE MBEYA “SAFARI HII HATUDANGANYIKI”

0

…………………………………………………………….

 Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbeya Mjini kwa tiketi ya CCM Dr. Tulia Ackson amefanya kampeni ya kunadi sera za chama chake katika kata ya Sinde jijini humo akiwaomba Wananchi kuwapatia dhamana ya kuwatumikia kwa nafasi za Urais, Ubunge na Udiwani katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika October 28, 2020.

Dr. Tulia akiwa katika kata hiyo amewaeleza Wananchi hao baadhi ya mambo ambayo CCM imeyafanya na ambayo inatarajia kuyafanya katika jiji hilo endapo watapigiwa kura za ndio>>>

”Ninapokuja hapa kwenu ndugu zangu mimi sio mgeni, kuna watu wanasikika huko wakisema kwamba tunakula kwa dada alafu tutalala sijui wapi… safari hii tunalala tulipokula. Kura yetu safari hii tutaipeleka kwenye maendeleo na maendeleo safari hii hapa Mbeya ni CCM tu”

“Mpaka hapa ninapozungumza na nyie baada ya kushuhudia mafuriko yaliyotupata katika baadhi ya maeneo ikiwemo kata ya Nzovwe, Isyesye, Igawilo, Sinde na mahali kwengineko mimi Mbunge wa kujiongeza nilishafanya connection na hadi hapa ninapozungumza na wewe umeshatengenezwa mpango kazi na imetumika Bilion moja nukta tatu kwa ajili ya kuhakikisha kwamba watu wanafanya usanifu ili miundombinu yetu ikae sawa, hatutaki tena mafuliko wala cha ndugu yake.”-Dr. Tulia Ackson

“Watu wa Mbeya safari hii tunaenda kwa kasi ya kujiongeza na kasi hii inatoka Chama Cha Mapinduzi pekee, pigieni kura zote CCM mjionee maendeleo yatakavyoinuka kwa kasi ya ajabu. Mtu akija kwenu kuwapiga propaganda muulizeni umetufanyia nini kabla ya kuja hapa kuomba kura?”-Dr. Tulia Ackson