Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kushoto akimnadi mgombea
Udiwani wa Kata ya Tangasisi Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa
kampeni
MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu ambaye pia ni Waziri wa
Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto akiwatubia wananchi wa
Kata ya Tangasisi wakati wa mkutano wake wa kampeni
KATIBU
wa UWT mkoa wa Tanga Sophia Nkupe akimuombea kura Mgombea Ubunge wa
Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu wakati wa mkutano huo
KATIBU Mwenezi wa CCM wilaya ya Tanga Lupakisyo Kapange akmuombea kura Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu
Msanii Mchina Mweusi akitumbuiza wakati wa kampeni hizo
MWENYEKITI
wea Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga Nassoro Makau akiwa na Mjumbe wa
Baraza kuu la UVCCM Taifa Mbaruku Asilia wakifuatilia mkutano wa mgombea
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu
Muwania
Udiwani viti malumu Tarafa ya Pongwe Mecha Goodluck akionyesha dole
wakati akiwa kwenye mkutano wa mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM)
Ummy Mwalimu
MUWANIA Udiwani wa Viti Maalumu Tarafa ya Pongwe Mecha Goodluck Matile akimuombea kura mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kulia wakati wa mkutano huo |
MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akiwa ameshika mtoto mara
baada ya kumaliza mkutano wake wa kampeni Kata ya Tangasisi
Umati mkubwa wa wananchi waliofurika kumsikiliza mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kata ya Tangasisi Tanga
Umati mkubwa wa wananchi waliofurika kumsikiliza mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kata ya Tangasisi Tanga
Umati mkubwa wa wananchi waliofurika kumsikiliza mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kata ya Tangasisi Tanga
Team Ummy Mwalimu wakiwa kwenye mkutano wa hadhara Kata ya Tangasisi
Msanii wa mziki wa Bongofleva Mwandeya akitumbuiza wakati wa kampeni hizo |
Msanii Kasimu Mganga akitumbuiza wakati wa mkutano huo
WAVUVI
Jijini Tanga wamehaidiwa kupatiwa neema ya kusaidiwa kupata dhana za kisasa
ikiwemo kuimarisha umoja wao ili waweze kupata mafanikio makubwa kupitia sekta
hiyo.
Hayo
yalibainishwa na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu wakati wa
mkutano wake wa kampeni Kata ya Tangasisi Jijini Tanga.
Alisema
kwamba ataimarisha umoja huo ili wavuvi waweze kuvua kisasa hatua ambayo
itawasaidia kuweza kupata samaki na kuweza kujikwamua kiuchumi wao na jamii zao
na hatimaye kukuza kipato chao
“Ndugu
zangu wavuvi nitahakikisha mnapata dhana za kisasa lakini pia kuimarisha umoja
wenu katika kata ya Tanga sisi na Jiji lote la Tanga muweze kupata mikopo isiyo
na riba na kununua vifaa vya uvuvi vya kisasa”Alisema
Akizungumzia
suala la fidia ya barabara Kata ya Tangasisi hadi Mwahako alisema tayari
alikwisha kuongea na Meneja wa Wakala wa Barabara Mkoa wa Tanga
(Tanroad) na tathimini inaendelea ikikamilika watu wote ambao wapo
barabarani watapata
malipo.
“Ndugu
zangu ninatambua hapa Tanga sisi hadi Mwahako kuna suala la fidia ya Barabara
suala hili tayari nimekwisha kuzungumza na Meneja wa Tanroad Mkoa wa Tanga tayati
tathimini inaendelea ikikamilika watu wote mliopo barabarani mtapata malipo
yenu”Alisema
Hivyo
aliwaomba wamchague kwa sababu ya uchungu alionao wa kuionga Tanga iweze kusonga
mbele huku akiwataka wampe kuwa nyingi za ndio kwa sababu amedhamiria
kuibadilisha Tanga.
Awali
akizungumza katika mkutano hyo Katibu wa UWT Mkoa wa Tanga Sophia Nkupe aliwaomba
wapiga kura kumchagua mgombea ubunge wa Jimbo
la Tanga Ummy Mwalimu kwa sababu amelelewa na jumuiya hiyo.
“Lakini
pia Ummy Mwalimu ni tunu kubwa tulioipata na kiongozi jasiri mwenye mafanikio
hivyo wananchi hatupaswi kufanya makosa kwa kuipoteza”Alisema
“Ndugu
zangu Ummy Mwalimu ni tunu kubwa tuliopata hivyo wananchi na wana Tanga
hatupaswi kufanya makosa wakati wa uchaguzi mkuu tumpeni kura nyingi za ndio
aweze kuilipatisha Jiji letu kutokana na mipango mizuri aliyonayo “Alisema
Katibu
huyo aliwaomba wananchi hao kuhakikisha wana mpa kura za kishindo Rais Dkt John
Magufuli ,Ummy Mwalimu na Diwani ili waweze kuchochea kasi ya ukuaji wa
maendeleo kwao