Home Siasa UMMY MWALIMU AHAIDI KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI JIJINI TANGA

UMMY MWALIMU AHAIDI KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI JIJINI TANGA

0

MGOMBEA Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akiwahutubia wananchi wa kata ya Maweni Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni

Normal
0

false
false
false

EN-US
X-NONE
X-NONE

/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-qformat:yes;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin-top:0in;
mso-para-margin-right:0in;
mso-para-margin-bottom:10.0pt;
mso-para-margin-left:0in;
line-height:115%;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,”sans-serif”;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;
mso-bidi-font-family:”Times New Roman”;
mso-bidi-theme-font:minor-bidi;}

MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu akiwahutubia wananchi wa
kata ya Maweni Jijini Tanga wakati wa mkutano wake wa kampeni
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mstaafu Hamisi Mkoba akizungumza kwenye mkutano huo ambapo aliwataka wananchi hao kumchagua Ummy Mwalimu
KATIBU Mwenezi wa CCM wilaya ya Tanga Lupaskiyo Kapange akimuombea kura Ummy Mwalimu wakati wa mkutano huo
Mwenyekiti Mstaafu wa Umoja wa Vijana Mkoa
wa Tanga (UVCCM) Abdi Makange
MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu kushoto akimnadi mgombea Udiwani wa Kata ya Maweni (CCM) Joseph Calvas wakati wa mkutano huo
 

WANANCHI wakifuatlia mkutano huo

MGOMBEA
Ubunge wa Jimbo la Tanga (CCM) Ummy Mwalimu amehaidi kumaliza tatizo la migogoro ya ardhi
katika kata ya Maweni Jijini Tanga endapo akichaguliwa kwenye uchaguzi mkuu
utakaofanyika mwezi Octoba mwaka huu kwa kuhakikisha wananchi wanapata haki.

Ummy
ambaye ni Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto aliyasema
hayo wakati wa mkutano wake kampeni uliofanyika mtaa wa Kange Kata ya Maweni
Jijini Tanga.

Aliwataka
wampe mamlaka ya kuwa mwakilishi wao ili kuweza kukomesha migogoro hiyo kwa
kuhakikisha wananchi wanapata haki ikiwemo wale waliopo kwenye maeneo yenye
migogoro wanafanyiwa urasimishaji kwa bei inayoshikika na sio beii kubwa.

“Nipeni
mamlaka ya kuwa mwakilishi wenu,nipeni mmlaka ya kuwa msemaji wenu,mamlaka ya
kuwa kiongozi wenu migogoro ya ardhi tutaikomesha katika kata ya Maweni
hususani kuhakikisha wananchi wanapata haki “Alisema

“Ikiwemo
wananchi waliipo kwenye maeneo yaliyo kuwa na mgogoro eneo la Jaribu tena  pamoja na maeneo ya Kasera wanafanyiwa
urasimishaji kwa bei inayoshikika na sio bei kubwa hili nalibeba wana Maweni
naombeni mniamini mnitume nikawatumikie”Alisema

Akizungumzia
kwa upande wa sekta ya Afya ,Ummy alisema kwamba sekta hiyo kwenye nchi hii ni
moja ya sekta iliyopata mafanikio makubwa kwenye nchi yetu ikiwemo kwenye Jiji
la Tanga.

“Nafahamu
hatujajenga zahanati na vituo vya afya kwenye baadhi ya kata na maeneo yetu
lakini tumehaidi kwenye ilani endapo mtanichagua mimi na Rais Dkt John Magufuli
tutajenga miundombinu ya kutoa huduma za afya”Alisema 

 ” Ikiwemo zahanati na vituo vya
afya katika maeneo  kwa kuzingatia
Geografia na eneo husika idadi ya watu pamoja na mzigo wa magonjwa kwa hiyo nikipita
tutakaa na diwani tupange vipaumbele wapi tuweke zahanati wapi tujenge kituo
cha Afya”Alisema

 

Alisema
kazi kubwa imefanyika katika utoaji wa huduma za afya na kubwa ambalo bado hatujakamilishwa
ni kuhakikisha wananchi wengi wanajiunga na bima ya afya ili waweze kupata
huduma za matibabu bila kikwazo cha fedha.

 

“Kwenye
hili naomba mniamini ni jambo kubwa ambalo Rais Magufuli amedhamiria
kulitekeleza kwa miaka mitano inayokuja kuhakikisha wana Maweni,wana Tanga
,Watanzania wanapata bima ya Afya kubwa ili kuweza kupata huduma bora za Afya bila
kikwazo cha fedha”Alisema

 

Alisema
pia amedhamiri kuleta mapinduzi ya kweli ya kiuchumi  na kijamii katika Jiji la Tanga hivyo wampe
heshima ya kuwa mbunge wao ili aweze kuchochea kasi ya ukuaji wa maeneo kwao na
jamii zinazowazunguka.

 Awali
akizungumza wakati wa kampeni hizo Mwenyekiti Mstaafu wa Umoja wa Vijana Mkoa
wa Tanga (UVCCM) Abdi Makange alisema baada ya Ummy Mwalimu kabla ya kuchaguliwa
kuwa mbunge wa viti maalumu mkoa wa Tanga katika Hospitali ya Mkoa wa Tanga
Bombo wakina mama walikuwa wakijifungua watoto njiti watatu lazima mmoja
anakufa kutokana na kukosekana kwa vifaa.

Alisema
kutokana na uwepo wa tatizo hilo walilazimika kumfuata Ummy Mwalimu
akawapelekea vifaa ambavyo vimekuwa mwarobaini mkubwa wa kumaliza tatizo hilo
na hivi sasa hakuna mtoto njiti anayefariki kwenye hospitali hiyo.