Home Mchanganyiko IGP SIRRO AONGEZEWA MWAKA MMOJA KUONGOZA SHIRIKISHO LA WAKUU WA POLISI MASHARIKI...

IGP SIRRO AONGEZEWA MWAKA MMOJA KUONGOZA SHIRIKISHO LA WAKUU WA POLISI MASHARIKI MWA AFRIKA EAPCCO

0

Mwenyekiti wa Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa Afrika (EAPCCO) ambaye pia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro (Pichani) akifuatilia mkutano mkuu wa 22 wa mwaka uliofanyika kwa njia ya mtandao (video conference) katika mkutano huo IGP Sirro ameongezewa mwaka mmoja kuongoza Shirikisho hilo la Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa Afrika. Picha na Jeshi la Polisi.

**********************************

18/09/2020 JIJINI DODOMA

Shirikisho la Wakuu wa Polisi Mashariki Mwa Afrika (EAPCCO) wamemtaka Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kuendelea kuwa mwenyekiti wa Shirikisho hilo kwa kipindi kingine cha mwaka mmoja.

Uamuzi huo umetolewa leo na nchi 14 wanachama wa Shirikisho hilo kupitia mkutano wake mkuu wa mwaka uliofanyika kwa njia ya mtandao (video conference) ambapo Wakuu hao waliona kutokana na kuibuka kwa ugonjwa wa Corona kumesababisha mambo mengi ya shirikisho hilo kutokamilika kwa wakati.

Hata hivyo IGP Sirro amesema kuwa, hadi sasa Shirikisho hilo limepata mafanikio makubwa huku akieleza kuwa katika kipindi cha 2021 wamejipanga kutekeleza yale ambayo hayakuweza kufikiwa na watahakikisha kuwa nchi wanachama wanaweza kubadilishana uzoefu na kufanya mafunzo ya pamoja ya mbinu za medani.