Home Mchanganyiko MAGUFULI AAGIZA MWALIMU MKUU WA SHULE YA BYAMUNGU ISLAMIC KUACHIWA NA POLISI

MAGUFULI AAGIZA MWALIMU MKUU WA SHULE YA BYAMUNGU ISLAMIC KUACHIWA NA POLISI

0

…………………………………………………

Na Allawi Kaboyo Bukoba.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Taifa na mgombea Urais kupitia chama hicho Dkt. John Pombe Magufuli ameziagiza wizara ya TAMISEMI na wizara ya elimu kuhakikisha shule zote zinazoanzishwa hapa nchini kuzingatia masuala ya usalama kabla na baada ya kuanzishwa kwake.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo septemba 16,mwaka huu kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Gymkhana mjini Bukoba ambapo amesema kuwa

Shule zote nchini zinazoanzishwa zinatakiwa kuwa na mifumo sahihi za kiusalama kwa watoto pamoja na watumishi katika shule hizo.

Amesema kuwa kumekuwepo na ajali mbalimbali katika baadhi ya shule zikihusisha masuala ya moto huku vyanzo vyake vikiwa havieleweki.

Aidha amelitaka jeshi la polisi kumuachia mwalimu mkuu wa shule ya msingi Byamungu ambaye alishikiliwa baada ya bweni la wavulana katika shule hiyo kuteketea kwa moto ambao ulisababisha vifo vya watoto 10 na wengine kujeruhiwa.

“Mwalimu huyu hawezi kuwa na roho mbaya ya kuwaua watoto wetu ambao amekuwa akiwalea kama watoto wetu kwa miaka mingi, tunapomshikilia tunaendelea kumuongezea uchungu maana nayeye ni mzazi na alianzisha shule kwaajili ya kuwasaidia watanzania, hivyo nikuombe mkuu wa Mkoa Kupitia jeshi la polisi muachieni mwalimu huyu.” Amesema Magufuli.

Rais Magufuli ameongeza kuwa mwalimu huyo hata akiwa nje ya mahabusu ya polisi anaweza kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kuliko kuendelea kumshikilia.

Mnamo usiku wa kuamkia septemba 14, shule ya Byamungu islamic primary iliyopo wilayani Kyerwa bweni la wavula la shule hiyo liliteketea kwa moto na kusababisha vifo vya watoto 10 na wengine kujeruhiwa ambapo bweni gilo lilikuwa na wanafunzi 74.