Home Mchanganyiko EWURA YAWAPIGA MSASA WATAALAM WA MAJI NA KULETA MIONGOZO MIPYA

EWURA YAWAPIGA MSASA WATAALAM WA MAJI NA KULETA MIONGOZO MIPYA

0

Mkurugenzi wa Maji na Usafi wa Mazingira,Mhandisi Exaud Fatael,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitoa taarifa kuhusu Semina ya kuwajengea uwezo watumishi kutoka kwenye mamlaka za maji zilizopo kwenye mikoa na miradi ya kitaifa kuhusu mwongozo huo inayofanyika jijini Dodoma.

…………………………………………………….

Na.Alex Sonna,Dodoma

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imeanza kuwajengea uwezo watumishi kutoka kwenye mamlaka za maji zilizopo kwenye mikoa na miradi ya kitaifa kuhusu mwongozo huo.

Hayo yamesemwa leo jijini Dodoma na  Mkurugenzi wa Maji na Usafi wa Mazingira , Mhandisi Exaud Fatael  wakati akizungumza na waandishi wa habari katika semina ya kuwajengea uwezo watumishi wa mamlaka ya maji nchini.

Aidha Mhandisi Fatael  amesema kuwa wameandaa mwongozo wa kuondoa maji taka na taka tope kwenye maeneo yasiyo na mtandao wa maji taka.

Mhandisi Fatael ameeleza kuwa huduma ya maji taka inazalishwa kwenye makazi lakini hakuna mfumo wa kuondoa maji taka na kwamba katika Mamlaka hizo 11 sio kaya zote zimeunganishwa na mfumo.

Mhandisi Fatael amesema kuwa tope taka linazalishwa baada ya utaratibu wa kibailojia wa kuondoa uchafu katika kinyesi cha binadamu, ambapo mwongozo huo unaelekeza namna ya kutumika bila kuleta athari.

Pia Mhandisi Fatael ametoa wito kwa jamii kuhakikisha kuwa na choo bora ili kuondoa maji taka eneo la makazi ili kutopata maradhi.

Mhandisi Fatael ameeleza kuwa mafunzo hayo yanatolewa kwa Mameneja ufundi na wanaohusika na usafishaji maji kwenye mamlaka hizo ili kudhibiti ubora wa maji na uwezo wa katika usafi wa mazingira.

Hata hivyo Mhandisi Fatael amesema kuwa Majukumu ya mamlaka hizo za maji katika mwongozo huu, yametajwa kwneye Sheria namba tano ya mwaka 2019 ya maji safi na usafi wa mazingira, ambayo ilipitishwa Julai mwaka jana na kuandaliwa kanuni, na kama Mamlaka ikishindwa kutimiza wajibu wake sheria itachukua mkondo wake.