Home Siasa DKT. HUSSEIN MWINYI, JAWABU LA WAZANZIBAR

DKT. HUSSEIN MWINYI, JAWABU LA WAZANZIBAR

0
****************************************
Na Emmanuel J. Shilatu
Heka heka za kampeni zinazidi kushika kasi na Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi anazidi kuchanja mbuga kujinadi na kuelezea atawafanyia nini Wazanzibar.
Upatikanaji wake unatokana na hitaji walilonalo Wazanzibar kwa sasa. Kama walivyo wateule wengine wa Urais wa awamu saba zilizopita walichagulia kupitia vikao vilivyofanyika mkoani Dodoma. Kama ambavyo Dk. Shein ama Karume walivyopatikana ndivyo hivyo hivyo Dkt. Mwinyi alivyopatikana kupitia michakato ya vikao vilivyofanyika mkoani Dodoma, ni utaratibu wa kawaida kabisa.
Dkt. Mwinyi hajimwambafai kama Mtoto wa Rais bali anasimama yeye kama yeye kutokana na haiba aliyonayo ya uzalendo, uchapa kazi, ufuatiliaji,  ucha Mungu na kujichanganya kwake kwa Watu. Hakika, Dkt. Mwinyi ni jawabu tosha la mahusiano mema na kuondoa matabaka kwenye jamii kwani yeye ni Mwana jamii haswaa.
Dkt. Mwinyi amejipambanua nyakati zote kutoa majawabu ya kero na changamoto za Wazanzibar tofauti kabisa na wagombea wengine waliogeuza midomo yao kunadi sera za matusi, ghiliba, kashfa, dhihaka na kauli za kuvunja amani ya Wazanzibar.
Kama nilivyosema Dkt. Mwinyi ni jawabu ya changamoto ya Wazanzibar ambao wanatamani wapate Rais mkali wa kukemea na kupambana na rushwa na ufisadi, Dkt Mwinyi amevalia njuga na kuhaidi undava wa kupambana na Mafisadi na wala rushwa.
Wazanzibar wana kiu ya kumpata Rais atakaye tatua kero ya ajira. Dkt. Mwinyi ameeleza vilivyo namna atakavyozalisha ajira zaidi ya laki tatu kupitia kuboresha sekta ya kilimo, kuanzisha viwanda, kukuza uvuvi, kujenga bandari, mafuta na gesi kupitia uchumi wa bluu. Haya yote yameelezwa kwenye ilani ya uchaguzi ambayo Dkt. Mwinyi amehaidi kuisimamia utekelezaji wake.
Dk. Mwinyi amejionyesha atakuwa kinara wa kupambana na dhuluma, udhalilishaji wa Wanawake pamoja na Watoto kwa kuhakikisha haki, usawa, umoja na mshikamano wa Wazanzibar unadumishwa.
Hakika yajayo ni neema tupu na yanafurahisha kwani ukitazama sura, matamshi, mienendo aliyonayo Dkt. Mwinyi utagundua ana dhamira kuu moja nayo ni kuwatumikia Wazanzibar.