Home Mchanganyiko WAGANGA WA TIBA ASILI KUANZISHA VIWANDA VIDOGO VYA DAWA NA KUUZA NJE...

WAGANGA WA TIBA ASILI KUANZISHA VIWANDA VIDOGO VYA DAWA NA KUUZA NJE YA NCHI

0

Meneja wa SIDO Mkoa wa Njombe bwana Izidory Kihenze akizungumza wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa SIDO Mkoani humo 

Mkuu wa mradi huo Dkt. Faith Mabiki akisisitiza jambo kwa washiriki hao wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo ya siku mbili kwa waganga wa tiba asili na tiba mbadala wa mkoa wa Njombe.

Dkt. Magoloni mtabibu wa tiba asili akipokea cheti kutoka kwa Mkuu wa Mradi huo Dkt. Faith Mabiki mara baada ya kuhitimu mafunzo hayo.

Waganga hao wa tiba asili na tiba mbadala ambao ndio walikuwa washiriki wa mafunzo hayo wakifurahia kila mmoja sabuni waliyotengeneza kwa mikono yao wakati wa mafunzo hayo iliyotokana na kila mtu na mmea wake.

Mtabibu Flavian Nyakeji akizungumza na Waganga wa tiba asili na tiba mbadala walipokuwa kwenye ziara ya kuangalia namna mtabibu huyo alivyoweza kuanzisha shamba la mimea dawa  na hivyo kupunguza changamoto ya upatikanaji wa dawa hizo.

Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye mazoezi kwa vitendo wakati wakiatengeneza sabuni kutokana na dawa ambazo kila mmoja amekuja nayo kama njia ya kuongeza thamani ya dawa zao.

…………………………………………………………..

Waganga wa Tiba asili na tiba mbadala Mkoani Njombe wamekishuru Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA kupitia watafiti wake kwa kuwajengea uwezo wa namna ya kuongeza thamani ya dawa zao ili kuongeza kipato na hivyo kuahidi kufanya kazi zao kisayansi ili waweze kusafirisha dawa hizo kwenda nje ya nchi.
Wakiongea mara baada ya mafunzo ya siku mbili yaliyotolewa na SUA kupitia mradi wa uvumbuzi katika mimea dawa kwa ustawi wa Watanzania AGRILI kwa kushirikiana na Shirika la Viwanda vidogo SIDO mkoa wa Njombe Waganga hao wamesema elimu hii ni muhimu sana kwani inawatoa katika kuuza dawa kama mizizi na majani na sasa wamekwenda kuzifungasha kitaalamu ili kurahisisha usafirishaji na matumizi.
Akiongea kwa niaba ya washiriki wenzake Rosta Ndunguru amesema matumizi ya miti dawa yamesaidia sana katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona na hivyo kurudisha Imani kwa jamii juu ya matumizi ya tiba asili na tiba mbadala na kwamba mafunzo hayo yatasaidia kuimarisha mbinu zao za utoaji dawa na matumizi ya dawa hizo.
” Tumeona Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Watanzania kwenye matumizi ya miti dawa katika kupambana na Corona, ameamsha Imani kubwa sana kwenye matumizi ya miti dawa yetu na kwa mafanikio hayo imeonesha jamii kuwa dawa hizi zinasaidia sana hivyo sasa tunakwenda kuziongeza thamani na kuzifungasha vizuri badala ya kumpa mtu mizizi sasa tunaweza tengeneza na kuzifungasha vizuri hata kusafirisha” Alisema Bwana Ndunguru.
Kwa upande wake Bwana Flavian Nyakeji amesema wakati umefika sasa waganga wa tiba asili na tiba mbadala kuachana na masharti magumu ya kurithi wanayowapatia wagonjwa wao kwakuwa yanawafanya watu wengi kuwaona matapeli hivyo waendelee kushirikiana na watafiti hao wa SUA kwenye kuboresha tiba.
Kwa upande wake Kiongozi wa mradi huo na Mtafiti Dkt. Faith Mabiki kutoka SUA amesema matabibu hao wakianza kutumia mbinu walizowafundisha katika kutoa huduma na wakatibu watu basi jamii itawaamini na hivyo kufanya biashara hiyo vizuri hasa ikizingatiwa kuwa sasa serikali imewatambua na kuhamasisha matumizi ya miti dawa nchini.
Ameongeza kuwa mafunzo hayo yanasaidia pia kuchangia juhudi za serikali za waganga wa tiba asili kufanya ramli chonganishi na mauaji mbalimbali ambayo mara nyingi vyanzo vyake huelekezwa kwao na hivyo kuifanya tiba asili kutumika kwa wingi na kuchana na madawa kama hayo yanayotoka nchi zingine wakati dawa zilezile lakini zilizoboreshwa.
Nae meneja wa SIDO mkoa wa Njombe bwana Izidory Kihenze ameahidi kushirikiana na waganga hao wa tiba asili na tiba mbadala katika hatua mbalimbali za uongezaji thamani wa dawa zao ili kuweza kufikia lengo la kufungasha vizuri na kwa ubora na kisha kuweza kusafirisha dawa hizo mikoa mbalimbali ya Tanzania nan je ya Tanzania.