………………………………………………………..
Kiasi cha shilingi bilioni kumi na tatu kinatarajiwa kutumika kwaajili ya kufanikisha ujenzi wa soko la kisasa kata ya Kirumba ili kuwainua wananchi kiuchumi na kuongeza pato la taifa.
Hayo yamesemwa na mgombea ubunge wa jimbo la Ilemela kupitia chama cha mapinduzi CCM Dkt Angeline Mabula wakati akizungumza na wananchi wa kata hiyo katika viwanja vya Bujumbura waliojitokeza kuhudhuria mkutano wake wa kampeni kwaajili ya kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuwa mbunge wa jimbo hilo kwa awamu ya pili ambapo amesema kuwa akichaguliwa atahakikisha anasimamia ujenzi wa soko la Kirumba kwa kiwango cha kisasa zaidi kuliko soko la kariakoo pamoja na miundombinu muhimu ya kuingilia sokoni humo ikiwemo ujenzi wa barabara zote zinazoingia ndani ya soko hilo kwa kiwango cha lami
‘.. Niwape siri moja tunalo soko letu la Kirumba, Soko lile linakwenda kujengwa kwa ghorofa na litakuwa na ukanda wa kufanyia biashara chini ya ardhi, Hili litakuwa bora kuliko lile la Kariakoo ..’ Alisema
Aidha Dkt Mabula akawataka wananchi hao kukiamini chama chake na kumpigia kura nyingi mgombea wa nafasi ya urais wa chama hicho Dkt John Magufuli kama shukran kwa namna alivyosaidia utatuzi wa migogoro ya ardhi ya muda mrefu iliyokuwa kero kwa wananchi hao ikiwemo mgogoro wa ardhi kigoto kati ya jeshi la polisi na wananchi ambao umeamriwa kwa jeshi la polisi kubaki na eneo kidogo wakati eneo lililobaki likichukuliwa na wananchi na kumilikishwa, mgogoro wa ardhi Lukobe kati ya jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ na wananchi wa mtaa huo ambapo uthamini umefanyika na wananchi wameanza kulipwa fidia, mgogoro wa rdhi Nyagunguru Ilemela ambapo wananchi wameanza kulipwa fidia.
Akimkaribisha mgombea huyo meneja kampeni wa CCM jimbo la Ilemela Ndugu Kazungu Safari Idebe amekemea upotoshwaji unaofanywa na baadhi ya wagombea kutoka vyama pinzani na kutoa lugha zisizofaa wakati wakiomba kura kwa wananchi huku akisisitiza kuwa suala la uchaguzi ni hiari ya wananchi kukichagua chama gani na mgombea gani hivyo kuwaomba kufanya siasa safi sanjari na kusisitiza amani na utulivu.