Home Uncategorized MAJALIWA AZINDUA KAMPENI ZA CCM WILAYANI RUANGWA

MAJALIWA AZINDUA KAMPENI ZA CCM WILAYANI RUANGWA

0

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na Wagombea Ubunge wa CCM, Salma Kikwete  wa Jimbno la Mchinga (wa pili kulia) na Hamida  Abdallah  wa Jimbo la Lindi wakati alipowasili kwenye kijiji cha Chinongwe wilayani Ruangwa, 

 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipowasili kwenye kijiji cha  Chinongwe wilayani Ruangwa,  kuzindua kapeni za CCM wilayani humo,

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akimsikiliza Mgombea  Ubunge wa CCM Jimbo la Mtama aliyepita bila kupingwa, Nape Nnauye wakati alipowaomba wananchi wampigie kura Rais Dkt. John Pombe Magufuli, wabunge na Madiwani wa CCM katika uzinduzi wa kampeni za CCM wilayani Ruangwa zilizoongozwa na Waziri Mkuu kwenye kijiji cha Chinongwe

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akishuhudia wakati Mbunge Mteule wa Viti Maalum Mkoa wa Lindi, Kijazi Yunus Mohamed alipopiga  magoti kuwaomba  wananchi wa Ruangwa wampigie kura Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Wabunge na Madiwani wa CCM katika uzinduzi wa kampeni za CCM wilayani Ruangwa ulioongozwa na Waziri Mkuu kwenye kijiji cha Nachinongwe, Septemba 11, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)