Home Siasa GWAJIMA KUAMSHA DUDE KAWE KESHO AKIZINDUA KAMPENI ZA UBUNGE

GWAJIMA KUAMSHA DUDE KAWE KESHO AKIZINDUA KAMPENI ZA UBUNGE

0
……………………………………………………………..
Na Magreth Mbinga 
Mratibu wa kampeni   ya ubunge Jimbo la kawe Ndugu Kolin mfinanga amewataka wananchi wa Jimbo hilo kujitokeza kwa wingi siku ya jumapili ya tarehe 13 katika uzinduzi wa kampeni ya ubunge.
Hayo ameyazungumza leo na kueleza kuwa   wampigie kura Askofu Gwajima kwasababu mbunge wa Jimbo hilo Halima Mdee ameshindwa kuleta maendeleo katika Jimbo hilo.
“Nilikuwa menija kampeni wa Halima Mdee lakini hakuweza kuleta maendeleo alikuwa anatafuta umaarufu wa chama chake”amesema Kolin.
Pia Andrew Samson  mwanachama na mwenyekiti wa mtaa wa Basiaya ambaye alikuwa mratibu wa kampeni  katika Jimbo la kawe alipokuwa chama Cha CHADEMA amesema wamejipanga kupata ushindi kwa Askofu Gwajima ili alikomboe Jimbo hilo.
Aidha amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya Jumapili ili kusikiliza sera za mgombea ubunge na mdiwani.