Home Mchanganyiko WAGANGA WA TIBA ASILI WAJENGEWA UWEZO WA KUONGEZA THAMANI YA DAWA ZAO...

WAGANGA WA TIBA ASILI WAJENGEWA UWEZO WA KUONGEZA THAMANI YA DAWA ZAO ILI KUBORESHA KIPATO.

0

Mkuu wa Mradi huo Dkt. Faith Mabiki akizungumza na Washiriki wa Mafunzo hayo juu ya lengo na mafunzo wakati wa ufunguzi rasmi wa mafunzo hayo.
Mgeni rasmi wa mafunzo hayo ambaye ni Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. David Ntahindwa wakati akifungua mafunzo hayo ya siku mbili kwa waganga wa Tiba asili na Tiba mbadala Mkoani Njombe.

Katibu wa shirikisho la la vyama vya Tiba asili Mkoa wa Morogoro Bwana Ramadhani Sanze akitoa ushuhuda wa bidhaa ambazo anatengeneza kutokana na mafunzo ambayo ameyapata kutoka kwa watafiti wa mradi huo.Washiriki wakimsikiliza Dkt. Faith Mabiki wakati akitoa utangulizi wa lengo la Mradi na mafunzo hayo.

Picha ya pamoja ya washiriki, Mgeni rasmi na watafiti kutoka SUA Mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
Mwanafunzi wa PhD kutoka SUA, Bw.Frank Rwegoshora akiwasilisha mada ya Utafiti wake kuhusu kemikali zinazopatikana kwenye miti Dawa mbalimbali.
Mwanafunzi wa PhD, Bw.David Credo akiwasilisha mada ya Utafiti wake kuhusu usugu wa Dawa na dozi.
Washiriki wa mafunzo hayo ambao ni waganga wa Tiba asili na Tiba mbadala kutoka Mkoa wa Njombe wakifuatilia mafunzo na mada mbalimbali zinazowashilishwa na watafiti kutoka SUA.
Mwanafunzi wa Shahada ya Uzamili bwana Said Babu akiwasilisha mada yake kuhusu kuhusu Utafiti wake wa  manufaa ya kiuchumi ya kuhifadhi mimea Dawa.

*************************************

Na: Calvin Gwabara – Njombe.

Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA katika Idara ya Kemia na Fizikia wamepongezwa kwa jitihada zao za wajengea uwezo Waganga wa Tiba asili na Tiba mbadala katika kuongeza thamani ya Dawa zao na matumizi endelevu ya miti Dawa yao ili kuboresha Tiba na kuongeza kipato.

Pongezi hizo zimetolewa na Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Njombe Dkt. David Ntahindwa wakati akifungua mafunzo ya siku mbili kwa Waganga hao wa Tiba asili na Tiba mbadala wa Mkoa wa Njombe yanayoendeshwa na SUA kupitia mradi wa Uvumbuzi katika mimea Dawa kwa ustawi wa Watanzania (GRILI) kwa kushirikiana na mradi wa kuongeza thamani kwa kemikali za SG kwa matibabu ya magonjwa ya binadamu na wanyama ( vaSPHAD).

Amesema katika kipindi cha hivi karibuni Dawa asili na Tiba mbadala imepata umaarufu Mkubwa kutokana na watu wengi sasa kuanza kuzitumia kwaaajili ya kutibu magonjwa mbalimbali lakini mazingira ya I tengenezaji wake na matumizi bado hayawekwa sawasawa hivyo kuwafanya watu wengine kusita kuzitumia kwa Kuhofia usalama wake.

“ Mafunzo haya yanayoendeshwa na watafiti wa SUA yataongeza thamani sana ya Dawa hizo lakini pia kuwa hakikisha usalama watumiaji kwakuwa watazingatia kanuni Bora za utengenezaji na ufungashaji ili kutoa Tiba unayo kusudiwa” Alisema Dkt. Ntahindwa.

Amefafanua kuwa mafunzo haya yamekuja muda muafaka hasa katika wakati ambao Serikali inasisitiza na kuzipa kipaumbele dawa za asili ili kuweza kutibu maginjwa mbalimbali ambayo yanaweza kutibika na dawa zetu badala ya kutegemea Dawa kutoka nje ya nchi wakati zinatoka kwenye miti na mimea ambayo tunayo hapa nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Mradi huo Dkt. Faith Mabiki amesema imefika wakati sasa Waganga wa Tiba asili na Tiba mbadala kunufaika na kazi zao wanazozifanya kwa kutibu jamii lakini Hilo litawezekana endapo waganga hao wataongeza thamani ya Dawa zao na kushiriki kwenye kulima miti Dawa hiyo ili isipotee kwakuwa wanaivuna kila siku.

Dkt. Mabiki amesema kuna Dawa nyingi zinatoka nje ya nchi hasa China na kuingia nchini na kutibu watu zikiwa zimeboreshwa vizuri wakati miti iliyotumika pia ipo hapahapa nchini na tunaitumia hivyo wakati umefika sasa na dawa zetu ziongezwe thamani na kuuzwa kwa wingi nchini na zingine kusafirishwa kwenda nje ya nchi.

Amesema mafunzo hayo yamewasaidia Waganga wa Tiba asili na Tiba mbadala wengi na sasa wanaweza kuongeza thamani kwa kuzifungasha vizuri na kuziiuza na kuziwekea taarifa muhimu za kemikali zilizo kwenye Dawa zao sambamba na namna ya kuzitumia na hivyo kuwawezeaha kuinua kipato chao.

Mkuu huyo wa Mradi amesema wamewajengea  ujuzi wa namna ya kutengeneza bidhaa kwaajili ya matumizi mbalimbali na sio kunywa pekee na hivyo kutengeneza sabuni zinaozotibu magonjwa mbalimbali mwilini na Pia kusaidia kurahisisha usafirishaji wa Dawa hizo tofauti na sasa ambapo wanasafirisha mizizi, Majani na magamba ya miti.

Ameongeza kuwa kwakuwa mahitaji ya miti Dawa yanaongezeka siku hadi siku kuna uwezekano wa miti mingi kupotea hivyo kama Mradi na watafiti wanaona Kuna umuhimu wa waganga hao wa Tiba asili na Tiba mbadala kuanza kulima miti na mimea hiyo ambayo ni muhimu katika kutoa Tiba na hivyo kusaidia kurahisha upatikanaji wake.

Dkt. Mabiki amesema kwenye mafunzo hayo wanawafundisha kanuni za msingi za usindikaji wa Dawa, Athari za usugu wa Dawa,kemikali zinazopatikana kwenye mimea Dawa mbalimbali nchini lakini pia namna ya kupanda mimea Dawa hiyo kwenye Mashamba na kustawisha.

Mafunzo hayo ya siku mbili yamewakutanisha waganga wa Tiba asili na Tiba Mbadala zaidi ya 20 na viongozi wao wa Mkoa Mzima wa Njombe kutoka Wilaya zote za Mkoa huo.