Home Siasa MAJALIWA AMUUNGANISHA MGOMBEA WA UBUNGE CCM MOSHI MJINI NA MTIA NIA AMBAYE...

MAJALIWA AMUUNGANISHA MGOMBEA WA UBUNGE CCM MOSHI MJINI NA MTIA NIA AMBAYE HAKUTEULIWA

0

Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM wa jimbo la Moshi Mjini, Priscus Tarimo  (kushoto) akikumbatiana  na mtia nia wa uteuzi wa CCM katika kugombea nafasi hiyo ambaye hakuteuliwa , Ibrahim Shayo wakati Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowakutanisha kwenye jukwaa kuu na kuwasihi wavunje ukimya. Ibrahim alitamka hadharani kuwa atamuunga mkono mgombea wa CCM Tarimo. Walikuwa katika mkutano wa kampeni uliohutubiwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa Majengo mjini Moshi.

Mgombea ubunge kwa tiketi ya CCM wa jimbo la Moshi Mjini, Priscus Tarimo  (kushoto)  na mtia nia wa uteuzi wa CCM katika kugombea nafasi hiyo, Ibrahim Shayo wakiudhihirishia  umma kuwa wapo pamoja wakati Mjumbe wa Kamati Kuu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowakutanisha kwenye jukwaa kuu na kuwasihi wavunje ukimya. Ibrahim alitamka hadharani kuwa atamuunga mkono mgombea wa CCM Tarimo. Walikuwa katika mkutano wa kampeni uliohutubiwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa Majengo mjini Moshi.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akisalimiana na mtia nia wa  uteuzi wa CCM katika kugombea nafasi ya ubunge jimbo la Moshi Mjini, Ibrahim Shayo ambaye alitamka hadharani kuwa atamuunga mkono Mgombea wa CCM katika jimbo hilo, Priscus Tarimo.  Mheshimiwa Majaliwa alikuwa katika mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Majengo mjini Moshi.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwakutanisha kwenye jukwa kuu, mgombea ubunge wa CCM jimbo la Moshi Mjini, Priscus Tarimo  (katikati) na mtia nia aliyeomba uteuzi wa CCM katika  jimbo hilo lakini hakuteuliwa, Ibrahim Shayo ambaye alitamka hadharani kuwa atamuunga mkono mwenzake Tarimo. Mheshimiwa Majaliwa alikuwa katika mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Majengo mjini Moshi,

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi   nakala ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025 mgombea ubunge wa CCM wa jimbo la Moshi Mjini, Priscus Tarimo katika mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Majengo mjini Moshi, Septemba 6, 2020. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)