Home Mchanganyiko PROF.SHEMDOE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI YA UWEZESHAJI BIASHARA JIJINI DODOMA

PROF.SHEMDOE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI YA UWEZESHAJI BIASHARA JIJINI DODOMA

0

Mkurugenzi idara ya Mtangamano wa Biashara, Ally Gugu, akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya uongozi, katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki Shemdoe na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dr. Mwinyi Talib Haji, kikao kimefanyika  jijini Dodoma.

Katibu Mkuu, Prof. Riziki Shemdoe katika picha ya pamoja na wajumbe walioshiriki kikao cha kamati ya uongozi kilichofanyika jijini Dodoma.

Katibu Mkuu Prof. Riziki Shemdoe akiwa na baadhi ya wajumbe mara baada ya kikao cha kamati ya uongozi kilichofanyika jijini Dodoma.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Dr. Mwinyi Talib Haji akizungumza wakati wa kikao cha kamati ya uongozi kilichofanyika  jijini Dodoma.

………………………………………………………………

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Riziki S. Shemdoe  ameongoza kikao cha Kamati ya Uongozi (Steering Committee) ya Uwezeshaji Biashara kilichofanyika   jijini Dodoma.
Lengo la kikao hiki lilikuwa ni kujadili utekelezaji wa maelekezo ya mkutano wa kwanza
wa kamati hiyo uliofanyika tarehe 13 Februari 2020.
Masuala yaliyojadiliwa na kuidhinishwa ni pamoja na hadidu za rejea (ToR) za kamati
ya kitaifa ya uwezeshaji biashara, Maeneo ya kundi A, B na C ya mkataba wa
uwezeshaji biashara wa Shirika la Biashara la Dunia (WTO TFA) ambayo yatawasilishwa sekretarieti ya WTO kabla ya tarehe 22 Septemba, 2020.
Utekelezaji wa masuala mengine ya biashara nje ya mkataba wa uwezeshaji biashara,
utekelezaji wa mpango mwelekeo (Roadmap) wa miaka mitano (2020/21 – 2024/2025)
na mpango kazi (Action Plan) ya mwaka 2020/2021. Aidha, Kamati imetoa maelekezo
ya maboresho ya Mfumo wa taarifa za ufanyaji biashara (National Trade Information
Module) kabla ya kufanyiwa uzinduzi rasmi.